Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Utangulizi
Kipindi cha ukoloni, watawala wakishirikiana na wamisionari (waliokuwa wanaeneza dini tofauti na zile za asili), walifanya kazi kubwa sana kuwaaminisha wenyeji kwamba matumizi ya Tiba asili ni ushirikina, na ni dhambi!
Kampeni hii ilienda sambamba na ujenzi wa hospitali na vituo vya Afya. Kwa kiasi kikubwa kampeni hizi zilifanikiwa, kwani hata baada ya kupata Uhuru, wananchi wengi ikiwa ni pamoja viongozi wa serikali waliendelea kuamini zaidi tiba za kisasa zinazopatikana katika hospitali, na vituo vya afya kuliko zile za asili.
Hadi miaka ya 1980, katika mahospitali na vituo vya afya, kulikuwa na mabango yaliyochorwa picha tatu; moja ikiwa ni ya daktari akiwa na vitendea kazi vya hospitali, ya pili ikiwa ya mganga wa jadi akiwa na mizizi na vitendea kazi vyake, na ya tatu ikiwa ni ya mgonjwa akiwa anaelekea kwa daktari, huku akimkwepa mganga wa jadi, huku akimwambia, ''Sizitaki dawa zako, kwani hazina kipimo''.
Ingawa mtizamo huu hasi dhidi ya tiba asili, ulianza kubadilika hapo baadaye, na hata kufikia hatua ya serikali kujumuisha tiba asili katika hospitali za rufaa, kama Muhimbili, KCMC, na Bugando; bado wataalamu wengi wa Afya pamoja na wananchi hawaamini sana katika tiba asili. Hii ina maana kwamba, kasumba iliyopandikizwa na wakoloni bado IPO vichwani mwa watu wengi mpaka sasa.
Tiba Asili na Tiba Mbadala Zinatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO)
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (World Health Organization - WHO)..(2019), mwaka 2005, WHO ilichapisha ripoti juu ya Sera na taratibu za kitaifa kuhusiana na tiba asili kutokana na utafiti wa kwanza wa kidunia katika Tiba Asili na Mbadala (Traditional & Complementary Medicine - T & CM).
Sambamba na mkakati wa WHO wa Tiba Asili wa 2002 - 2005 na mkakati wa WHO wa Tiba Asili wa 2014 - 2023, na maazimio ya mikutano husika, nchi wanachama zilichukuwa hatua kati ya 2005 na 2018, kukuza usalama, ubora na ufanisi wa Tiba Asili na Mbadala (TA & M).
Taarifa inaendelea kusema, nchi wanachama zilichukuwa hatua za kujumuisha Tiba Asili na Mbadala (TA & M) katika mifumo ya Afya (hasa katika huduma za Afya) kwa kuandaa Sera, mifumo ya kisheria na mipango mkakati ya kitaifa juu ya bidhaa, huduma na wahudumu wa Tiba Asili na Mbadala (TA & M). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, asilimia 88 ya nchi wanachama (ambazo ni sawa na nchi wanachama 170, Tanzania ikiwepo) zimetambua matumizi ya TA & M.
Serikali ya Tanzania Inatambua Tiba Asili na Mbadala
Tanzania kama moja ya nchi mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO), imeridhia maazimio mbalimbali kuhusiana na swala la tiba asIli na mbadala; ndio maana ina sera, taratibu na sheria, na tayari kuna Baraza la Tiba Asili na Mbadala, chini ya wizara ya Afya.
Serikali imeenda mbali zaidi, kwani imesajili na inaendelea kusajili watoa huduma wa Tiba Asili na mbadala, pamoja na dawa husika. Vilevile, serikali imejumuisha tiba Asili na mbadala katika hospitali zake kubwa za rufaa kama Muhimbili, KCMC na Bugando.
Kasi ya Matumizi ya Tiba Asili na Mbadala Tanzania ni Ndogo.
Pamoja na ukweli kwamba serikali inatambua Tiba Asili na Mbadala, bado kasi ni ndogo sana, kwani kuna hospitali na vituo vya Afya vilivyosambaa katika wilaya takriban 160 nchini, ambavyo vilipaswa kuwa na huduma ya Tiba Asili na Mbadala, lakini mpaka leo ni hospitali 7 tu zenye huduma hizi tena kwa kiasi kidogo.
Kwa mujibu wa Jarida LA Mtandaoni la Wizara ya Afya/Toleo No. 19, Mei 2024, Tiba Asili & Mbadala ni moja kati ya vipaumbele 10 vya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2024/25, ambapo kiasi cha Sh. 1.5 bilioni kimetengwa. Hii ni sawa na asilimia 0.12 ya bajeti ya jumla ya Sh. 1.3 trilion.
Hii inadhihirisha kwamba Tanzania bado hatujaweza kutilia mkazo hii dhana ya TA & M, ukilinganisha na taifa la India.; kwani kwa mujibu wa tovuti ya news.un.org>stoty>2022/03, Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) na Serikali ya India wametia saini makubaliano ya kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Tiba Asilia cha WHO.
Kituo hiki cha maarifa cha kimataifa cha tiba asili kinachofadhiliwa na uwekezaji wa dola milioni 250 (sawa na Sh. za kitanzania takriban 650 bilioni) kutoka kwa Serikali ya India, kinalenga kutumia uwezo wa dawa asilia kutoka kote ulimwenguni kupitia sayansi na teknolojia ya kisasa ili kuboresha afya ya watu na sayari dunia.
India ni nchi inayoendelea, lakini imeweza kuwekeza kiasi kikubwa hiki katika TA & M; hii inadhihirisha kuwa imejitoa kwa dhati kuhakikisha huduma hii inafika mbali kwa manufaa ya watu wake na wa dunia kwa ujumla.
"Kwa mamilioni ya watu duniani kote, dawa za jadi ni kimbilio la kwanza la kutibu magonjwa mengi," amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus akiongeza "kuhakikisha watu wote wanapata matibabu salama na yenye ufanisi ni sehemu muhimu ya dhamira ya WHO, na kituo hiki kipya kitasaidia kutumia nguvu za sayansi ili kuimarisha msingi wa ushahidi wa tiba asilia''.
Tanzania tuitakayo katika Dira ya 2025 - 2050
Serikali inapaswa kuweka miundombinu ya kuwezesha kujumuishwa kwa TA& M pamoja na wahudumu wake katika hospitali na vituo vya Afya kote nchini.
Serikali ipunguze au iondoe kabisa gharama ya kupima dawa asili, ili kuvutia matabibu wengi zaidi kupima bidhaa zao, na hivyo kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa ambazo hazijahakikiwa.
Serikali iwekeze katika utafiti wa TA & M pamoja na mafunzo ya mara kwa mara kwa Matabibu wa TA & M.
Serikali itakapoongeza uwekezaji katika Tiba Asili na Mbadala, sambamba na kuboresha Afya za wananchi, itapunguza matumizi ya mamilion ya fedha za kigeni kununua dawa kutoka nje ya nchi, na pia watu wengi (kila wilaya) wataajiriwa na kujiajiri. Kwa ujumla, jitihada hizi zitachochea ukuaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa.
HITIMISHO
Tunaweza kufanya mapinduzi katika sekta ya Afya na ya kiuchumi, kama serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla watazingatia kwa dhati Tiba Asili & Mbadala.
Rejea
Jarida la Mtandaoni la Wizara ya Afya/Toleo Na. 19, Mei 2024; Afya Habari.
news.un.org>story>2022/03
World Health Organization (2019), WHO Global Report on Traditional and Complementary Medicine
www.michuzi.co.tz

Upvote
12