Tiba asili

Tiba asili

Bennie 369

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
713
Reaction score
534
1.UNGA WA MKAA.
Unaweza kuupata kutoka kwenye mti wa mkuyu,kifuu cha nazi,msonobari na mkaratusi (eucalyptus .

Jinsi ya kutayarisha:~
Choma kifuu cha nazi hadi kiwe mkaa na usage uwe unga. Kwa hiyo miti yake niliyoitaja utatumia magome yake. Chukua kijiko kimoja kikubwa cha unga wake (wa mkaa)alafu uchanganye na maji safi ya uvuguvugu (uwe kama ujiuji)kikombe kimoja na unywe kabla ya kula.

Inatibu magonjwa yafuatayo :~
*kutapika ,kuhara damu ,kuharisha, vidonda vya tumbo, macho,kunywa sumu, tindikali, uvimbe,tatizo la usagaji chakula,kiungulia na kuumwa na nyoka.
(Kwa aliyeumwa na nyoka shona kimfuko cha kitambaa cheupe na uweke kijiko kimoja kikubwa cha huo unga kisha uweke na maji kidogo ili uloane )kisha funga kwenye jeraha, na kila baada ya saa moja fungia nyingine na pia uendelee kumpa mgonjwa kikombe kimoja cha maji yaliyochanganywa na huu unga wa mkaa kama nilivyoelezea hapo juu kila baada ya saa moja, inaweza ukafika hospital na sumu imekwisha yote. Kwa wale waliokunywa sumu tumia njia ya kunywa kikombe cha maji ya uvuguvugu. Na wale wenye tatizo la macho wanatakiwa waifunge hii dawa kwenye kimfuko kama nilivyoelezea hapo juu kisha wafungie/kuweka juu ya jicho kwa siku tatu mfululizo wakati wa usiku .

2. NDEVU ZA MAHINDI
Hizi hupatikana kwenye mhindi wenyewe,

Jinsi ya kutayarisha :~
Chukua ndevu za mahindi za kutosha, chemsha maji lita mbili kisha ziloweke kwa dakika kumi na tano, chuja na unywe bilauri mbili kila siku kwa siku tano.
Inatibu magonjwa yafuatayo :~
Figo, kibofu cha mkojo, inasaidia kwa wale wenye uvimbe wa miguu,shida katika kukojoa hasa wanaume wazee, na kwa watoto wanaokojoa kitandani wape na wataacha kukojoa.

3.CASTOR TREE .
Chukua mizizi yake na weka juu ya mkaa na ikishapata joto mama mwenye ujauzito/mimba aitafune atajifungua salama na mfuko utatoka bila matatizo(kondo la nyuma) na pia kwa kuchemsha majani yake inasaidia kurudisha mgongo unaotoka nje (rectum)

4.MGAGANI
Majani yake ni dawa ya sikio hasa lenye usaha, kwa kusafisha kila siku jioni kwa siku tano.

5.HOLYTHISTLE
Hutibu ugonjwa wa akili na kupoteza fahamu , chuma Majani nusu kilo chemsha maji lita mbili kisha uyaloweke haya Majani kwa dakika tano, tumia kikombe kikubwa cha nusu lita kutwa mara tatu kwa juma, kisha pumzika kwa juma. Kama ugonjwa ni wa mda mrefu unaweza ukaendelea.

6.MBUYU.
Unatibu homa,malaria, kifua kikuu, kukohoa pumu. Chukua magome yake loweka ndani ya maji safi baridi, tumia nusu kikombe kutwa mara tatu.
 
Back
Top Bottom