TIBA MBADALA:Kunywa maji yamoto ni tiba yamagonjwa mengi

Mad Scientist

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
215
Reaction score
77
Kuna tiba nyingi za kitabibu,
zilizogawanyikaa katika makundi
mbalimbali. Kuna zile za hospitali
ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini
kuna tiba ambazo kwa ushauri wa
daktari hata wewe unaweza
kuziandaa bila kutumia gharama
kubwa.
Moja ya tiba hizo ni kunywa maji
ya moto. Kwa mujibu wa
wataalamu wa afya maji moto
yanatibu magonjwa mengi ikiwemo:
Figo, kutoa sumu mwilini,
kuyeyusha mafuta tumboni,
kurahisisha mzunguko wa damu,
kuondoa sumu kwenye ubongo na
kusafisha haja ndogo.
Kunywa maji ya moto kila
unapotaka kwenda kufanya kazi ya
nguvu au mazoezi iwe kama kinga
na inashauriwa kila siku anywe
glasi nane ili kutoa taka na kila
kisichotakiwa kubaki mwilini,
kupitia jasho.
Wadau wa afya wanasema kuwa
ni vyema pia kunywa maji ya moto
yenye ndimu au limao kabla ya
kifungua kinywa ili kurahisisha
mfumo wa mwili kwa siku nzima.
Pazi Mwinyimvua, Mtaalamu wa
Chakula na Lishe kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, anasema
kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji
wa chakula na mafuta mwilini,
hivyo kutokana na umuhimu huo ni
vyema kunywa maji ya moto
yatakayofanya kazi haraka na kwa
ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.
Anaitaja faida nyingine ya kunywa
maji ya moto kuwa ni kutoa sumu
zilizopo kwenye mishipa ya fahamu
na kuisaidia figo kufanya kazi
kikamilifu, tofauti na maji baridi
ambayo yanagandisha na
kuilazimisha figo kuyeyusha
kwanza na kisha kuchuja
Anashauri umuhimu wa kunywa
maji moto kabla ya kufanya
mazoezi kuwa ni kujiandaa kwa
ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa
sumu, hivyo yakiwa ya moto
yakifika yanaanza kufanya kazi
moja kwa moja, kuliko yakiwa ya
baridi yanaweza kusumbua kwa
kuwa ni lazima yapate joto la mwili
kwanza kabla ya kuanza kufanya
kazi.
“Ukiachilia kusubiri yachemke pia
ni kumuepusha mtumiaji na hatari
ya kuumwa tumbo kutokana na
kunywa maji ya baridi bila kuweka
kitu tumboni na kwenda kufanya
mazoezi kitu kinachoweza
kuzidisha maumivu au maji
kucheza wakati wa kukimbia kama
mazoezi ya kukimbia. Lakini
yakiwa ya moto ni kama
umekunywa chai au kula chakula
cha kawaida” anasema
Mwinyimvua.
Mwinyimvua anaongeza kuwa maji
ya moto ni mazuri hata kwa kupata
choo, kwa vile kinarahisisha
uyeyushaji na uchambuaji wa
kinachotakiwa na kisichotakiwa,
wanaokunywa ya baridi wana
uwezekanao mkubwa wa kupata
haja kubwa kwa shida.
Vilevile Mwinyimvua anashauri
kuwa ni vyema kunywa maji moto
yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe
na kuwa vuguvugu na kuongeza
limao na asali mbali na kuongeza
ladha, asali na limao vina faida
kiafya.
Gayl Canfield , RD, Mkurugenzi wa
Lishe kutoka katika Kituo cha
Biashara cha Pritikin Longevity
kwenye Mji wa Miami , Florida
nchini Marekani, anasema kuwa
kunywa maji ya uvuguvugu au ya
moto ni vyema kwa kuwa hufanya
kazi moja kwa moja kutokana na
hali ya tumbo kuwa na joto muda
wote.
Canfield anasisitiza, “Maji ni
muhimu kwa mwili wako, yakiwa
ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa
yanatoa rangi ya njano ya mkojo na
kuufanya uwe msafi na wenye
rangi angavu”.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…