TIBA MBADALA:Kunywa maji yamoto ni tiba yamagonjwa mengi

Mad Scientist

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
215
Reaction score
77
Kuna tiba nyingi za kitabibu,zilizogawanyikaa katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.

Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo:

Figo, kutoa sumu mwilini,kuyeyusha mafuta tumboni,kurahisisha mzunguko wa damu,kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.

Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini,kupitia jasho.

Wadau wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Pazi Mwinyimvua, Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini,hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.

Anaitaja faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.

Anashauri umuhimu wa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kuwa ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu, hivyo yakiwa ya moto yakifika yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

"Ukiachilia kusubiri yachemke pia ni kumuepusha mtumiaji na hatari ya kuumwa tumbo kutokana na kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kitu kinachoweza kuzidisha maumivu au maji kucheza wakati wa kukimbia kama mazoezi ya kukimbia. Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula cha kawaida" anasema Mwinyimvua.

Mwinyimvua anaongeza kuwa maji ya moto ni mazuri hata kwa kupata choo, kwa vile kinarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa,wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.

Vilevile Mwinyimvua anashauri kuwa ni vyema kunywa maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza limao na asali mbali na kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya.

Gayl Canfield , RD, Mkurugenzi wa Lishe kutoka katika Kituo cha Biashara cha Pritikin Longevity kwenye Mji wa Miami , Florida nchini Marekani, anasema kuwa kunywa maji ya uvuguvugu au ya moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya tumbo kuwa na joto muda wote.

Canfield anasisitiza, "Maji ni muhimu kwa mwili wako, yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenyerangi angavu".
 
huwezi kunywa maji ya moto hadi yapoe na kuwa vuguvugu mkuu. Nimekuwa nikinywa hivyo kwa muda ni kweli naona improvements.
 
Nimeipenda ubarikiwe


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Joto kiasi gani la maji yanaongelewa hapa? Nilidhani ni maji ya vuguvugu ila baada ya kusoma nimeona yametenganishwa vuguvugu na maji ya moto. Je, yanayoongelewa hapa yanatakiwa yawe ya moto kama chai?

watu8 ukipata wasaa, kwa hisani yako, unaweza kutoa mchango mkuu!
 
Last edited by a moderator:

Hapa yanaongelewa maji ya moto. Kwa watanzania wengi walivyozea, kunywa maji tupu yasiyo na majani ya chai wala sukari ni ajabu. lakini kama unaweza kunywa chai basi fanya kuondoa majani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu yawe moto au vuguvugu yote ni sahihi tu, kitu cha muhimu ni kwamba maji ya baridi hayana faida kiafya zaidi tu ya kupoza mwili kwa haraka.

Hii article imegusia mambo mengi sana muhimu ikiwemo hilo la kunywa maji mara baada ya kuamka.

 
Last edited by a moderator:
Mkuu yawe moto au vuguvugu yote ni sahihi tu, kitu cha muhimu ni kwamba maji ya baridi hayana faida kiafya zaidi tu ya kupoza mwili kwa haraka.

Hii article imegusia mambo mengi sana muhimu ikiwemo hilo la kunywa maji mara baada ya kuamka.

Shukrani mkuu, ntaanza kupiga kikope kimoja cha maji kama ya chai bila sukari wala majani. Ntaendelea kadri muda utakavyoruhusu. Nakubaliana na wewe kuhusu maji ya baridi sema ndio hivyo tena mambo ya Sprite (Tii kiu yako)

Ubarikiwe kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…