Tiba ya bawasiri nje ya hospitali

DENAMWE

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2019
Posts
862
Reaction score
871
Nina jamaa yangu ambaye aliugua bawasiri akafanyiwa upasuaji.

Kuna madai kuwa baada ya upasuaji ugonjwa huu unarudi.

Wanadai kuwa ukitibiwa hauponi moja kwa moja. Unarudi.

Naomba ushauri na maelekezo ya FIBA sahihi.
 
Mafuta ya habat sawdah a.k.a. black seed yanauzwa kati ya elfu 4 au 3 anapakaa hayo tu basi
 
Kabla ya kufanyiwa upasuaji je nyama zilikua zinatoka nje akizirudisha. Zinarudi. Nimeuliza hvyo maana mpak kafanyiwa upasuaji tatizo lilikuw lishakuw kubwa au yeye aliamua tu kwenda kufanyiwa oparesheni

Kabla ya opareshen waga wanatumia mafuta au cream kulainisha nyama hzo sasa kama kasha fanyiw upasuaj ni vgumu sa nya kurudi tena itachukua muda mrefu sana au zisirudi kabisa.

Mafuta na cream wanazapaka nazo havitakiwi kupakw kwa muda mrefu huez kusababisha infection yaan itilafu kwenye seheemu hyo au vidonda

Awe anakula mbogamboga ili kufanya chookiwe kilaini kisije kikaleta mchubuko
 
God Forbid aiseee!! Ni hatari sana
 
Dawa yake ni ku control chakula tu

Jiepushe na constipation na diarrhoea

Vyakula hakikisha unatumia mboga mboga na matunda kwa wingi, unywe na maji.

Aina ya choo unachotumia, angalia choo cha kukaa kinaweza kukupa urahisi bila kupata hiyo shida mara kwa mara.

Ukizingatia hayo utabaki na bawasiri yako ila haitakupa shida yeyote.
 
Chizi karogwa tena.
 
BAWASILI INASABABISHWA NA ;

GENETICS. **** familia nyngine watu hupata tu na tatizo hilo

OBESITY uzito kupita kiasi

PRESHA KUBWA KWENYE MWILI hasa wanyanyua vyuma au kukohoa sana kwa muda mrefu au wa kati wa haja kubwa kutumia nguvu nyingi inafa nya nyama kuchanika

MIMBA nazo huongeza kupatikana kwa bawasisiri hasa pale mtu anpojifungua hutumia nguvu nyingi kusukuma ambazo husababisha nyama za tumbo kuweka weaa line

MAGONJWA YA MUDA MREFU AMBYO MTU UVIMBA TUMBO
 
Huo sio ugonjwa. Ni mwili unajirepair. Kinachotokea hapo ni kama vile utokee ufa kwenye ukuta au kwenye ardhi halafu mtu ajazie kifusi au ujazie sementi.

So kinachotokea hapo ni kwamba unapopata constipation choo kikakwa kigumu halafu haujapata choo muda mrefu, then mwili bowel inajikusanya sababu inashuka taratibu katika utumbo kuja njia ya haja kubwa.

Mwisho wa siku mzigo unakuwa mkubwa na kumejikusanya na unatakiwa kutoka wote. Unapofika muda wa kutoka misuli ya ndani ya section hiyo karibia na njia ya haja kubwa hupush kwa nguvu mzigo utoke.

Sasa njia kwasababu ni ndogo na hupitisha vitu laini then lazima kutatokea hali ya kuchanika kidogo ili namna gani vipi ipite.

Sasa ukishachanika ndipo tissue za lile eneo huwa zinawahi kujazia zile vidonda kama vile nyufa inavyojazwa sementi. Sasa kile unachoita uvimbe actually si uvimbe bali ni mwili unarepair sehemu iliyochanika kwa kutumia tissue mpya na kupajaza. Pakijaa hapataweza rudia kuwa kama zamani kwasababu tayari tissue zimejaza ile nafasi sasa ndio kinatokea kile kijinyama.

Ukienda kufanyiwa upasuaji mwili tena utadetect kuwa umeondoa kitu so zitarudi tena marambili ya ile ya kwanza ili kurepair hiyo damage mpya ya kutolewa kile kinyama kilichojaza.

So kwa kifupi huu sio ugonjwa wala si tatizo kuwa na hiyo kitu unachotakiwa ni kuzingatia lishe bora ya mboga za majani kwa wingi, maji kwa wingi na matunda katika diet yako choo kiwe na fiber na ulaini wa kutosha hautasikia hizo hemorrhoids hata mara moja.

Ila narudia tena zile si ugonjwa ni mwili unajirepair.
 
Uzungu uzungu mwingi sana miaka hii ndio maana hata matatizo nayo yanakuwa si yale yaliyozoeleka.
 
Kwenye ujauzito (neno mimba tunatumia kwa wanyama sio binadamu) hapo swala si wakati wa kujifungua (neno kuzaa tunatumia kwa wanyama sio binadamu) bali swala ni wanawake wajawazito hupatwa na constipation sana wakati wa ujauzito ila sio kwamba kupush tu siku moja wanapata bawasili.
 
Mwenye tatizo hilo anicheki PM nitampa namba ya jamaa anatibu kwa miti shamba
 
layman language. ujauzito ni kama risk/associated factor
 
Nina jamaa yangu ambaye aliugua bawasiri akafanyiwa upasuaji.
Kuna madai kuwa baada ya upasuaji ugonjwa huu unarudi.
Wanadai kuwa ukitibiwa hauponi moja kwa moja.
Unarudi.

Naomba ushauri na maelekezo ya FIBA sahihi.
Hello habari yako Mkuu dawa ya maradhi ya bawasiri ipo nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako uguw apole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…