Habari zenu wakuu..
Kwa anaefaham dawa au tiba ya kichunjua anifahamishe. Ni aina ya kikovu kidogodogo au mara nyingine huwa km kipele kisichokwisha hata km utakikuna au kukikwangua kwa kucha hutoa yale magamba ya juu na baada ya muda kinatokea tena. Kwa mm hakiniwashi ila huwa nina tabia ya kukikuna. Ninacho kichwani kwa mda wa miaka kumi sasa. Kwa anaefaham tiba yake naomba anisaidie..
Natanguliza shukran zangu za dhati kwa atakaenisaidia
Bibi yangu alikuwa nacho mguuni baada ya muda fulani kikageuka kuwa kidonda kwenda hospitali akaambiwa ni kansa na imeshafika pabaya, sasa ameshafariki kutokana na kansa ambayo imetokana na hicho kichunjua, hivyo nakushauri nenda kaonane na daktari.