Tiba ya malimao na kitunguu saumu haijaanza leo kuleta utata

Tiba ya malimao na kitunguu saumu haijaanza leo kuleta utata

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakuu kuna huyu mama alikuwa waziri wa Afya wa Africa kusini kipindi cha Thabo Mbeki, alikuwa anaitwa Manto Tshabalala Masimang.

Huyu alikuwa anapinga kuwa VVU haisababishi UKIMWI na akawashauri wananchi watumie malimao na vitunguu saumu kutibu UKIMWI. Mbeki alikuwa nyuma yake naye akiamini VVU havisababishi UKIMWI. Dunia ilimpigia sana kelele.

Alikataa kuanzisha mpango wa ARV na alitafuna pesa za UKIMWI. Nilipomsoma huyu maza niliona wasauzi ni vilaza wa mwisho lakini leo nimekumbuka kupitia stori yake.

Hivi inakuwaga ni nini kwa wanasiasa kujidai kujua sayansi ya tiba? Zuma naye amewahi sema kuoga baada ya ngono kunazuia maambukizi ya UKIMWI! Mtikila naye alisema kufunga siku tatu mfululizo kunatoa VVU mwilini. Trump naye anasema klorokwini inatiba Corona!

Nafikiri kuna kipindi wanasiasa wanatakiwa kukaa pembeni na kuacha wataalamu wafanye kazi zao.
 
Hatari nianyoiona huko mbele ni mwendo wa PUD za kutosha... tusubir tu.
 
Kuna mda nawaza sana kuhusu hili JANGA ila kuna wakati nasahau,
Sasa nikipitiaga tu hapa JF mawazo yanarudi upya na hofu.

Sijui hata nifanyaje?
 
Back
Top Bottom