Tiba ya maumivu ya kifua

Tiba ya maumivu ya kifua

Kaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
745
Reaction score
372
Ndugu zangu, leo ni siku ya pili nina maumivu ya kifua (kinauma kwa ndani) lakini sibanji na wala sikohoi mfululizo. Siwezi kuvuta pumzi (deep inhale), niki/inama/inuka/lala au nikijigeuza nahisi maumivu makali ya kifua kwa ndani. Muda huu naandika nimeshindwa kulala na kwetu huku zahanati ziko mbali na usalama ni mdogo kabisa.

Naomba kujuza tatizo na tiba yake tafadhali.
 
Nipo above 30, sijawahi ugua kifua kwa namna maumivu haya navyoyapata, usiku nimetumia Tangawizi kuitafuna ndo kidogo nafuu lakini bado. Yawezekana sio sisi wawili tu hali hii imetukuta
 
Hata mimi kifua kinasumbua sana hasa usiku, hewa navuta kwa taabu halafu kinauma kwa ndani.Sijui tatizo huwa nini
 
Hata mimi kifua kinasumbua sana hasa usiku, hewa navuta kwa taabu halafu kinauma kwa ndani.Sijui tatizo huwa nini

Ni awamu hii tu ndiyo umepata hayo maumivu au ni mara kwa mara? na kama ni tatizo la muda mrefu unaweza kuelezea ni kipindi/majira gani ya mwaka ugonjwa huu unakupata? na je, unapumua kwa shida na ni sauti gani ikutokayo kwenye mapafu pindi unapopumua? kuna aina yoyote ya mafua inakuijia km kiashiria cha kuanza kuumwa hicho kifua?
Umeshawahi kuulizia kama mna historia ya Asthma ktk ukoo wako au wa mama?

Nijibu hayo maswali kiufasaha then nitakupa ushauri nini cha kufanya.

Cc Kaka na Mahesabu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom