Tiba ya uvimbe chini ya taya

Tiba ya uvimbe chini ya taya

ween

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
414
Reaction score
129
Matumaini yangu mu wazima,

Ninahitaji msaada wa haraka, nimetokewa na uvimbe mdogo size kama tunda la mzabibu ni kidogo kwa nje hakionekani isipokuwa nikishika sehemu hayo ya taya ndipo nikibinya taratibu nasikia kinauma. Ila pasipo kukitafuta nikakibinya sisikii maumivu kabisa, ninatafuta vizuri naachama vizuri nageuka vizuri.

Ninaomba kujua hili tatizo gani na linasababishwa na nini. Pia naomba nipatiwe tiba yake.
 
hakuna namna nenda hospitali kuna kipimo kimaitwa fnac au biopsy
fnac waatoa sampo ya maji maji kwenye uwo uvimbe inapimwa kama majibua yataonekana hakuna kitu.
ndo unafanya biopsy wanatoa huo uvimbe unapimwa kujua umeletwa na nini

but before that angalia kama unashida kwenye meno au infection kwenye maskio pia inasababisha uvimbe
 
Mkuu nenda hospital haraka kwa vipimo zaidi, inaweza kuwa ni tussue dis formation ya kawaida auvya cancer
 
Watanzania wengi nikiwemo na mimi tumejijengea mfumo wa kuogopa kwenda kupima ikiwa ni kutokana na hofu ya majibu nitakayopatiwa huenda ugonjwa ukawa mkubwa usio weza kuumudu matibabu yake hapo ndipo kichwa kitawaka moto ukizingatia ufakara umekuzunguka kweli natamani ila wachanijichange mfukoni kwanza,........pia nikiwa nasubiri mfuko utune naomba mwenye tiba ya kiasili anielekeze
 
pia angalia uvimbe ukianza kua mgumu hausogei ukiuguza ni hatari sana nenda hospitali mkuu
kufanya biopsy kweli ni ghali maana kufanya operation kutoa uvimbe pamoja na kwenda kuupima
 
Matumaini yangu mu wazima,

Ninahitaji msaada wa haraka, nimetokewa na uvimbe mdogo size kama tunda la mzabibu ni kidogo kwa nje hakionekani isipokuwa nikishika sehemu hayo ya taya ndipo nikibinya taratibu nasikia kinauma. Ila pasipo kukitafuta nikakibinya sisikii maumivu kabisa, ninatafuta vizuri naachama vizuri nageuka vizuri.

Ninaomba kujua hili tatizo gani na linasababishwa na nini. Pia naomba nipatiwe tiba yake.
Ushauri wa msingi uende hospital ukamuone dkt wa meno ambao taya ni eneo lao LA ubobezi atakupatia msaada kulingana na tatizo lako
 
Back
Top Bottom