Benokolongokonongose
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 213
- 52
Nikiwa kwenye basi nilikaa na mgavi(distributor)kutoka kampuni ya Amezcua wenye anuani hii www.qnet.net. Amenionesha bidhaa mbalimbali za asili akisema hayina madhara. Baadhi ya bidhaa hizo ni kama vile Chi pendant ambayo unavaa kama cheni shingoni kwaajili ya kukupa nguvu. Akasema kuwa mtu akivaa anaweza akapigana na watu hata 40 na wasimuweze. Akaonesha na bio disc akisema imasaidia kutakasa maji na ukinywa sana maji hayo huponya hata kansa na UKIMWI. Akaendelea kuonesha bidhaa kadha wa kadha.
Akanishawishi niwe mgavi na kwamba kampuni yao inamtambua mteja na kumpa kadi ya discount akinunua mzigo mara 1 tu na mtu unaingiza faida kuliko forever Products na GNLD. Pia unatoka kimaisha ndani ya miezi 3 tu, Kwa walio na ufahamu juu ya hili bidhaa hizi kweli hazina madhara?Na faida ni kubwa zaidi?