#1. KUKOSA CHOO (CONSTIPATION)
Hali ya kupata choo mara chache au kupata choo kigumu, au ugumu wa kupitisha choo.
VISABABISHI
Kukosa choo kunatokana na sababu tofauti tofauti ikiwemo :
- Lishe yenye upungufu mkubwa wa nyuzi nyuzi (fibers)
- Unywaji mdogo wa maji.
- Matumizi ya baadhi ya dawa mf. Antibiotics
- Huzuni na msongo wa mawazo.
- Ujauzito kutokana na mabadiliko ya homoni.
- Mwili kukaa muda mrefu bila kujongea
- Bawasiri.
- Na nyinginezo.
Pale sababu ya tatizo inapojulikana inatakiwa itibiwe.
TIBA
(i) ULAJI wa matunda na mboga za majani kwa wingi pamoja na kupunguza ulaji wa nyama na ngano iliyokobolewa.
(ii) KUNYWA maji kwa wingi.
(iii) UWATU (FENUGREEK)
Matumizi ni kijiko cha chai 1-2 mara 2-3 kwa siku kwenye maji vuguvugu
- Upo wa unga na WA mbegu, wa unga ni rahisi zaidi kwa matumizi
- Unapatikana kwenye maduka ya viungo na ya dawa za asili.
ANGALIZO : Haitakiwi kutumika na mjamzito.
- Jitahidi kunywa maji kwa wingi unapotumia uwatu kwa kuwa una kawaida ya kunyonya maji kwa wingi ili kusaidia mjongeo katika mfumo wa chakula.
(iv) UKWAJU (TAMARIND)
Matumizi : Unaweza kutumia kama juisi kwa kadiri ya mahitaji
ANGALIZO : Tumia kiasi, matumizi yaliyopitiliza huweza kuchochea kiungulia/acid reflux
TIBA zifuatazo zinatakiwa kutumika kama chaguo la mwisho kwa tatizo sugu na kwa muda mfupi kwa kuwa huwa zina nguvu sana na zinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kama zikitumika kwa muda mrefu.
(v) MAFUTA YA NYONYO (CASTOR OIL)
Matumizi ni 5ml mara 2-3 kwa siku.
USITUMIE zaidi ya siku 8.
ANGALIZO : Haitakiwi kutumika na mjamzito.
(vi) SANA MAKKI (SENNA)
Matumizi : Kutegemeana na maelekezo ya daktari/tabibu wako.
ANGALIZO : Usitumie zaidi ya wiki moja.
• WADAU WOTE MCHANGO WENU NI WENYE KUHITAJIKA.
• MWENYE NYONGEZA, MAREKEBISHO KARIBU SANA.