Ticket za Usafiri wa Train kukatwa kwa Utambulisho wa S/mitaa...

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
Leo Nimepita Ofisi ya Shirika la Reli ya kati na kukuta kitangazo cha Maka pen nyekundu,kuwa Wale wote wanaoenda kukata ticketi waende na utambulisho wa vitu vifuatavyo....
1.Barua kutoka serikali ya mtaa,kijiji.
2.kitambulisho cha kupigia Kura/leseni.
3.Hati ya kusafiria.
Bila hvyo hupati ticketi wasukuma,wakigoma mpo hapo.

Nlipouliza sababu hyo mmoja wafanyakazi alijibu ni kutaka kuwabaini wakimbizi.

Nimeshndwa kuweka picha ya tangazo lao natumia simu,Invisibo anipe msaada wa kuziwe hapa zipo 3.
 
Kwani wao UHAMIAJI,NIDA nadhani wanatapatapa pia kuingilia majukumu ya watu tu,nchi ya ujanjaunja naona nafasi ya kuwapiga jambajamba wananchi imewadia.
 
Ni mbinu nzuri ya kupunguza watembeaji nchi hii bila utaratibu
 

Du! Hii sasa ndio yenyewe. Hapa ukitaka kusafiri lazima uage mtaani kwenu, vinginevyo hupati ticketi. Vipi kuhusu wanaosafiri kwa kutumia mabasi na magari binafsi? au jamaa wanakaba hadi Ubungo pale?
 
Du! Hii sasa ndio yenyewe. Hapa ukitaka kusafiri lazima uage mtaani kwenu, vinginevyo hupati ticketi. Vipi kuhusu wanaosafiri kwa kutumia mabasi na magari binafsi? au jamaa wanakaba hadi Ubungo pale?

Aisee nahisi wapo kwenye mchakato,wakianza na ubungo duuh
 
Ndio kwanza leo nisikie usafiri wa ndani ya nchi kuhitaji kibali cha serikali. Hivi sie Watanzania wazima kweli?

Kwa nini tunazidi kuongezeana adha kwenye maisha yetu ya kila siku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…