TICTS walipewa Mkataba wa miaka 20. Je, DP World Mkataba wao ni muda gani?

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,562
Reaction score
15,985
Swali la msingi liko hapo.

TICTS walipewa miaka 20, waliposhindwa na mkataba kuisha wamenyimwa nyongeza ya mkataba. Je, hao DP World mmewapa muda gani? Ili nao wakishindwa tutafute mwekezaji mwingine na kama watafanikiwa waongezewe mkataba kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hoja ya watanganyika wengi ni kufahamu muda wa mkataba ni upi? Serikali hamna sababu ya kuzunguka jibuni tu kua mwekezaji mpya kapewa kwa muda fulani na akishindwa kama ilivo kwa TICTS ndio hatoongezewa mkataba.

Hatutaki mikataba ya ajabu ya kutufunga hapana na hilo haliwezekani kabisa.
 
Watasaini mikataba mingi lazima nchi ifaidike milele Tz haihami upo siku zote.
 
Watasaini mikataba mingi lazima nchi ifaidike milele Tz haihami upo siku zote.

Hapana sio kweli na lazima waelewe wananchi asilimia kubwa hawawaungi mkono kwenye hilo
 
Mkataba ulishasainiwa tangu october 2022.

Hizi kelele zetu hazitasaidia kitu, serikali walishausoma pamoja na mapungufu yoote tunayoyabaini, wakazibwa mdomo wasihoji kitu, wakasaini kuwa wameelewa, hawawzi kurudi tena na kudai kuna mapungufu, hawataeleweka kwa mwarabu.

Mbona hata misitu mwarabu amesaini kusimamia misitu yote kuendesha sijui kufanya nini na jeshi kule arusha twiga wanaondoka kila siku mikataba ni mingi sana kwa waarabu kiufupi tumeisha uzwa labda tutafute njia ya kujikomboa.
 
DPW wamepewa Mkataba wa Maisha/milele.

Kwa kifupi ni kwamba Watanganyika tumeuzwa jumla julmla kwa Waarabu wa Dubai.
Extremely sad!

Who Bewitched black people in this world?😞😞😞😞😞
 
Ili ndio ccm hawataki kutolea majibu utasikia bado hatujatia makubaliano ya kimkataba ni upembuzi tuu.

Ata uvccm hawajui waseme nini, hii imesimama wakigusa wanaisikia kabisa, wakiinama inapenya yote mazima
 
Ili ndio ccm hawataki kutolea majibu utasikia bado hatujatia makubaliano ya kimkataba ni upembuzi tuu.

Ata uvccm hawajui waseme nini, hii imesimama wakigusa wanaisikia kabisa, wakiinama inapenya yote mazima

Wao waseme ni miaka mingapi hoja iishe sio blah blah za mara ni mou mara ni vile hata hawaeleweki
 
Hapo Hawataki kusema kabisa,ila mkataba wa Congo huo wanajua mpaka na muda wa mkataba,ila hapa Tz hawajui na wanashangilia tu,na ninaamini hata hapo bungeni mtu kama Msukuma ndio unaweza kusema eti alisoma huo mkataba,yy alikuwa anatetea asichokijua kulingana na Elimu aliyonayo,na ukishakuwa mjinga unaanza kuamini mambo ya kijinga jinga tu,Eti mbunge anasema pale bandarini Dubai mdada mmoja mdogo mdogo ndie anaye endesha mitambo kikubwa na anaamin Tanzania hao mabinti wenye uwezo huo hawapo,very poor argument, ww mbunge una tuhela tu hilo tu ndilo ulilonalo,watu wanapojadili mambo ya kisheria na kudadavua ww kaa kimya usaidiwe kuelewa taratibu mambo ya kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…