TID anasikitisha sana, apewe msaada wa haraka

TID anasikitisha sana, apewe msaada wa haraka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Umofia kwenu wanaJF,

Huwa sipendi kuzungumzia afya za watu,ukweli kwamba nakuwa sina vithibitisho vya ushahidi lakini kwa hili la TID naomba kulizungumzia.

Wiki mbili zilizopita niliudhuria sherehe ya THT kutimiza miaka 10, Venue ilikuwa Escape1, pale Mlalakuwa karibu na jeshi.

Wakati nipo kwenye mishe zangu za kucheki wachuchu nikakutana na mnyama TID,kwanza nilishangaa kumuona kwa jinsi alivyokuwa kakonda na mwenye wasiwasi.

Nilijaribu kumsogelea ili kumdadisi vyema lakini nikashtushwa na harufu ya pombe maarufu kama kiroba na alikuwa kashika glasi fulani aliyokuwa kahifadhia hiyo kitu.

Yaani muda wote TID alikuwa mtu wa kujitenga (Mpweke) peke yake huku akiwa na wasiwasi,Muda mwingi alikuwa akijikuna mikono,mashavu na sehemu ya shingo.

Kwa uzoefu wangu wa watumiaji ngada bila shaka jamaa alikuwa anasumbuliwa na madawa ya kulevya na pale alikuwa arosto.

Kwanza afya yake ni dhaifu sana alafu uso umechoka balaa na ana madoa doa mengi usoni.

PLS, watu wake wa karibu wangejitahidi kumsaidia TID, tutampoteza kama wale wale tuliowapoteza kwa matumizi haya ya ngada.

Alafu jamaa ni mtata sana ukimhoji kuhusu kutumia madawa ya kulevya.

Mwisho nawaomba msamaha wapenzi wa TID kwa kumsema vibaya ila kwa nia njema.

Wasalaam.

========

Hii ni interview ya TID na Sporah, TID alimind sana alipoulizwa kuhusu afya yake na matumizi ya madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kupitiliza.

Sporah: "hapa watu wanasema TID amepungua sana, kitu ambacho kinasikitisha amekuwa kama mtoto mdogo, kama ni pombe basi utakuwa unakunywa sana"

TID: sometimes i need to be who i want to be, no body tell me unapungua au haupungui, i wanna be flexible with my music with my work, i think this is the good look i need to look, i dont wanna be like any body, i wanna be special, am feet am healthy, i dont care what people think about me.

Sporah: but we care about you!

TID: its my weight, my life my health, if am good am good

Sporah: do u think you have a good health at the moment

TID: yeah am fine, am healthy

Sporah: i dont think your healthy though?

TID: are you my doctor? are you trying to be my doctor...
 
Last edited by a moderator:
Kwa hapa TID anatisha mno kivipi dogo??? Na hiyo ngada ni mdudu gani?
Tuondolee uharo hapa bwana.
 
Nimelazimika kufuata busara za SUPU YA MAWE. Kwa sababu nimeona na-reveal sana taarifa ambazo zilikuwa ni off-record, kitu ambacho kingeweza kujenga chuki baina ya msanii husika na watajwa. Asante pia kwa ushauri wako!

Itoshe!
Ni kweli ungejenga chuki, huyo dada watamtenga na kuanza kumwita snitch. mwamajinja mapunga kwa bahati mbaya hakutaja jina la sporah
 
Last edited by a moderator:
Jina usitoe coz youtube hiyo kitu ipo. Watanzania tuache uoga. Angalieni watu wa TMZ wanavyochana makavu live. Nyie vipi bhanaa. Aaaghhhr
 
Mleta thread yupo sahihi kabisa.TID kaharibika kwa sababu ya unga.Nilibahatika kuona show ya sporah alipokuwa hewani na TID,ni majanga na aibu.Mostly akiguswa kuhusu personal life alikuwa mkali kama Simba duh.Pia hata kiafya hayupo njema kabisa.In short the celebrity has all signs of teja.Tumuombee,Mungu amsaidie for sure.
 
Kwa wale wanaoulizia interview ya TID na Sporah (Sporah Show) Nimeiweka kwenye post ya kwanza. Wenye macho wataona jinsi mnyama alivyojichokea kwa afya mgogoro(Samahani).

Ukweli lazima usemwe ili tuokoe wasanii na muziki wa Tanzania kwa ujumla.

cc. Blog
 
Last edited by a moderator:
MR. CONFIDENT, Umenena vyema, wasanii asilimia kubwa wanatumia madawa japokuwa wakakataa kukiri. Sijui msaada gani wapatiwe ili kuondokana na hili tatizo.

Wanatumia wamejificha lakini wakishaharibikiwa ndio wa kwanza kuomba msaada wa pesa za matibabu na kadharika.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hapa TID anatisha mno kivipi dogo??? Na hiyo ngada ni mdudu gani?
Tuondolee uharo hapa bwana.

Kwako ni uharo lakini kwa wengine kunena kwangu ni msaada.Huenda hata wewe ni muathirika wa madawa ya kulevya ndio maana umeishia kunitukana. Nakuomba ukapate ushauri wa kitabibu na kifikra kwa wataalam.
 
Hata ray c akitaka kuwasaidia wanamtukana na kumpiga, sasa tutafanyaje?

View attachment 225471

Mfano ni Chid Benz, dada wa watu kwa moyo wa msaada akamuomba amsaidie jamaa kutokana na hali aliyokuwa nayo but akaambulia matusi pamoja na kipigo kikali.

Dada wa watu bila hiyana akamsamehe maana na yeye kapitia huko na anajua watu wa hivi wasivyopenda kuambiwa ukweli.

Sasa hivi Chid yupo? Angalia muonekano wake kwa sasa, Na sasa hivi ana kesi ya kukutwa na kete wakati akisafiri kuelekea kwenye show Mtwara.

Mungu aliamua kumuumbua baada ya kumdhalilisha Ray C kwa kumpiga.
 
Mleta thread yupo sahihi kabisa.TID kaharibika kwa sababu ya unga.Nilibahatika kuona show ya sporah alipokuwa hewani na TID,ni majanga na aibu.Mostly akiguswa kuhusu personal life alikuwa mkali kama Simba duh.Pia hata kiafya hayupo njema kabisa.In short the celebrity has all signs of teja.Tumuombee,Mungu amsaidie for sure.

Kama uliangalia kwa makini basi uligundua jamaa (TID) kadata, kwanza mimi nilimshangaa alivyoanza kumshambulia Sporah bila hata sababu ya msingi. Sporah alihoji kutokana na yale yanayosemwa mtaani,TID alichopaswa kusema ni kukanusha au kukiri na sio majigambo na ubabe alioonesha.
 
Mteja ni shoga wa pili, magari mengi bado hayajaanza kuwaka yakianza itakuwa mcharuko..madude siku hizi si ya mabongofleva peke yao ata mabongomuvi wamepokea kijiti. Tatizo la Mzee Warioba ni misosi anavunga misosi na vumbi bila misosi lazima utupambie magazeti. Na hasira zinamjia vipi maniga kibao wanakula madude alafu habari inakuwa mzee tu na watu wanawajua.
 
Binafsi, nilibahatika kukutana na msanii wa kike wa kurap aliyewahi kutamba enzi hizo (jina nalisitiri), maana alihamia kwa muda jirani na nyumba niliyokuwa naishi last year. She is too talkative, na ni aina fulani ya watu ambao ni rahisi sana kuzoeana nao, so tulizoeana na nilifanikiwa kumuuliza masuala flani flani hivi kuhusu Muziki na wasanii...

Katika maelezo ya bidada huyu, alisema wasanii wengi wanatumia ngada. Wengi sana. Na alisema muda ukifika tutawaona dhahiri. Nikamuuliza kwani wewe hujawahi kushtua? Akakataa kata kata, akadai yeye ana vitu vyake tu, ila ngada anaiheshimu kupindukia, anaiogopa kama Ukoma!

Hakuishia hapo, alisema wengi pia ni waathirika wa HIV, na alinitajia mpaka majina (nayahifadhi), na akasema muda ukifika kila kigawe lazima kitaguswa. Alikuwa akisisitiza Muda tu. Kwamba kila kitu kitakuwa wazi muda ukifika!

Kuhusu TID pia nilimuuliza...Hakunijibu, lakini akasema 'Kinondoni haifai'.. Alinitolea mifano mingi na ushahidi mwingi kuhusu wasanii wa Kinondoni coz yeye mwenyewe alitokea huko. Alitaja historia na matukio. Aliwataja mpaka wanasiasa wakubwa na wafanyabiashara wakubwa wenye majina (huwezi kuamini) ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa kuwaharibu wasanii..

Itoshe!

•Dude alishasema wasanii wa bongo movie na bongo fleva wengi wana ngoma,yupo sahihi.
•Kuhusu swala la ngada halina mjadala.
 
Binafsi, nilibahatika kukutana na msanii wa kike wa kurap aliyewahi kutamba enzi hizo (jina nalisitiri), maana alihamia kwa muda jirani na nyumba niliyokuwa naishi last year. She is too talkative, na ni aina fulani ya watu ambao ni rahisi sana kuzoeana nao, so tulizoeana na nilifanikiwa kumuuliza masuala flani flani hivi kuhusu Muziki na wasanii...

Katika maelezo ya bidada huyu, alisema wasanii wengi wanatumia ngada. Wengi sana. Na alisema muda ukifika tutawaona dhahiri. Nikamuuliza kwani wewe hujawahi kushtua? Akakataa kata kata, akadai yeye ana vitu vyake tu, ila ngada anaiheshimu kupindukia, anaiogopa kama Ukoma!

Hakuishia hapo, alisema wengi pia ni waathirika wa HIV, na alinitajia mpaka majina (nayahifadhi), na akasema muda ukifika kila kigawe lazima kitaguswa. Alikuwa akisisitiza Muda tu. Kwamba kila kitu kitakuwa wazi muda ukifika!

Kuhusu TID pia nilimuuliza...Hakunijibu, lakini akasema 'Kinondoni haifai'.. Alinitolea mifano mingi na ushahidi mwingi kuhusu wasanii wa Kinondoni coz yeye mwenyewe alitokea huko. Alitaja historia na matukio. Aliwataja mpaka wanasiasa wakubwa na wafanyabiashara wakubwa wenye majina (huwezi kuamini) ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa kuwaharibu wasanii..

Itoshe!

Wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa wakubwa ni kina nani?
Kinondoni mbunge wao tu Iddi Azzan alituhumiwa kuuza unga
huyo msanii sio Sister P?
 
Umofia kwenu wanaJF,

Huwa sipendi kuzungumzia afya za watu,ukweli kwamba nakuwa sina vithibitisho vya ushahidi lakini kwa hili la TID naomba kulizungumzia.

Wiki mbili zilizopita niliudhuria sherehe ya THT kutimiza miaka 10, Venue ilikuwa Escape1, pale Mlalakuwa karibu na jeshi.

Wakati nipo kwenye mishe zangu za kucheki wachuchu nikakutana na mnyama TID,kwanza nilishangaa kumuona kwa jinsi alivyokuwa kakonda na mwenye wasiwasi.

Nilijaribu kumsogelea ili kumdadisi vyema lakini nikashtushwa na harufu ya pombe maarufu kama kiroba na alikuwa kashika glasi fulani aliyokuwa kahifadhia hiyo kitu.

Yaani muda wote TID alikuwa mtu wa kujitenga (Mpweke) peke yake huku akiwa na wasiwasi,Muda mwingi alikuwa akijikuna mikono,mashavu na sehemu ya shingo.

Kwa uzoefu wangu wa watumiaji ngada bila shaka jamaa alikuwa anasumbuliwa na madawa ya kulevya na pale alikuwa arosto.

Kwanza afya yake ni dhaifu sana alafu uso umechoka balaa na ana madoa doa mengi usoni.

PLS, watu wake wa karibu wangejitahidi kumsaidia TID, tutampoteza kama wale wale tuliowapoteza kwa matumizi haya ya ngada.

Alafu jamaa ni mtata sana ukimhoji kuhusu kutumia madawa ya kulevya.

Mwisho nawaomba msamaha wapenzi wa TID kwa kumsema vibaya ila kwa nia njema.

Wasalaam.

========

Hii ni interview ya TID na Sporah, TID alimind sana alipoulizwa kuhusu afya yake na matumizi ya madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kupitiliza.

Ushauri wako ni mzuri. Hata hivyo. Hawa ma/vi superstars whatever they call themselves wanaposnza kubwia huwa na wanajua kabisa madhara ya madawa ya kulevya.

Isitoshe huwa wamezungukwa na ndugu jamaa marafiki pia wanaowauzia. Sasa inakuwaje watu hao hushindwa kuwadhibiti wakati wanaanza kuyatumia hadi wanafikia hatua mbaya? Na hapo ndipo utaanza kusikia kuwa msanii fulani asaidiwe hali yake si nzuri!

So watu walio/ wanafaidi pesa zake wanamtupa tena mtu wao! Na tatizo linahamishiwa kwa entire jamii!? Binafsi ni ngumu kuielewa. Waanze kwanza watu kama wazazi, kaka, dada, ndugu, marafiki na wauzaji wao ndipo wengine wafuatie.

After all kila mmoja huchagua aina na style ya maisha anayotaka kuishi.
 
Back
Top Bottom