Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Na Mwandishi Wetu
Wiki chache baada ya mwanamuziki mwenye heshima kubwa kunako Bongo Flava, Khaleed Mohamed TID kumvisha pete ya uchumba Miss Kinondoni the history aliyetajwa kwa jina moja la Kinana, anayetarajia kufunga naye ndoa soon, msanii huyo amepata pigo kubwa, Risasi Mchanganyiko linakuweka karibu naye...
Gazeti hili lilipenyezewa tipu ya kubomolewa kwa nyumba ya bosi huyo wa Top Band na familia yake, aliyokuwa anatarajia kuishi na mnyange huyo baada ya kufunga ndoa.
Risasi Mchanganyiko lilitia timu nyumbani kwa staa huyo anayetamba na songi la Asha kideoni, maeneo ya Sterio Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambapo lilipata chansi ya kushuhudia maafa hayo.
Akisimulia mkasa huo, mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake lichorwe kwenye peji hii alisema kwamba, wakazi wa eneo hilo wamekumbwa na ishu hiyo baada ya kupewa notsi ya kupisha ujenzi wa upanuzi wa Barabara ya Hananasifu unaotarajiwa kuchukua nafasi muda si mrefu.
Katika kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya bomoa bomoa kwa kutumia greda maalum, Top in Dar aliamua kutekeleza zoezi hilo mwenyewe kukwepa athari zingine ambazo zingeweza kutokana na uvunjaji huo aliodai utakuwa wa rafu.
Akifafanua ishu hiyo, Meneja wa Top Band, Khamis Dakota alilimbia Risasi Mchanganyiko kwamba, pamoja na vitu vingine, lakini Studio ya Top Records, mali ya TID ilivunjwa ambapo vifaa vyote vilihamishiwa katika nyumba ya familia ya msanii huyo iliyokuwa nyuma ya studio hizo.
Ni kweli, tumepata maafa, studio yetu ya Top Records imebomolewa, lakini kila kitu kimewekwa sawa hapo nyumbani. TID mwenyewe anamwachia Mungu ndiyo mtoa kheri, alisema Dakota.