TID apata pigo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Na Mwandishi Wetu
Wiki chache baada ya mwanamuziki mwenye heshima kubwa kunako Bongo Flava, Khaleed Mohamed ‘TID’ kumvisha pete ya uchumba Miss Kinondoni ‘the history’ aliyetajwa kwa jina moja la Kinana, anayetarajia kufunga naye ndoa ‘soon’, msanii huyo amepata pigo kubwa, Risasi Mchanganyiko linakuweka karibu naye...
Gazeti hili lilipenyezewa ‘tipu’ ya kubomolewa kwa nyumba ya bosi huyo wa Top Band na familia yake, aliyokuwa anatarajia kuishi na mnyange huyo baada ya kufunga ndoa.

Risasi Mchanganyiko lilitia timu nyumbani kwa staa huyo anayetamba na ‘songi’ la Asha kideoni, maeneo ya Sterio Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambapo lilipata ‘chansi’ ya kushuhudia maafa hayo.

Akisimulia mkasa huo, mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake lichorwe kwenye ‘peji’ hii alisema kwamba, wakazi wa eneo hilo wamekumbwa na ishu hiyo baada ya kupewa ‘not’si’ ya kupisha ujenzi wa upanuzi wa Barabara ya Hananasifu unaotarajiwa kuchukua nafasi muda si mrefu.

Katika kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya bomoa bomoa kwa kutumia ‘greda’ maalum, Top in Dar aliamua kutekeleza zoezi hilo mwenyewe kukwepa athari zingine ambazo zingeweza kutokana na uvunjaji huo aliodai utakuwa wa ‘rafu’.

Akifafanua ishu hiyo, Meneja wa Top Band, Khamis Dakota alilimbia Risasi Mchanganyiko kwamba, pamoja na vitu vingine, lakini Studio ya Top Records, mali ya TID ilivunjwa ambapo vifaa vyote vilihamishiwa katika nyumba ya familia ya msanii huyo iliyokuwa nyuma ya studio hizo.

“Ni kweli, tumepata maafa, studio yetu ya Top Records imebomolewa, lakini kila kitu kimewekwa sawa hapo nyumbani. TID mwenyewe anamwachia Mungu ndiyo mtoa kheri,” alisema Dakota.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…