TID apewa kichapo ka mbwa mwizi!

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,596
Reaction score
1,234


Mwanamuziki nyota wa Bongo flava ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa dansi, Khalid Mohammed ‘TID’, wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kudundwa hadi kutolewa nundu puani na mtangazaji wa Clouds TV, Cedou Ayoub a.k.a Babuu.

Tukio hilo la aina yake lililotokea wiki iliyopita kwenye kiota cha burudani Bongo pale Club Maisha na kushuhudiwa na watu kibao ambapo chanzo chake kikidaiwa ni kudaiana hela

Chanzo chetu kilimwaga umbea kuwa, siku ya tukio hilo TID alikuwa amealikwa kwenye uzinduzi wa albamu ya mwanamuziki Country Boy iliyokuwa inafanyika mjengoni humo, ambapo baada ya onesho hilo kuisha ndipo TID akiwa ‘mitungi’ alimfuata Babuu na kuanza ‘kumzingua’

Hata hivyo, chanzo chetu kiliendelea kueleza kuwa, baada ya walinzi wa ukumbi huo kuona hali tete ya uvunjifu wa amani waliwasihi watu hao kutoka nje kabisa ya ukumbi, huku mtangazaji huyo akiwaomba walinzi hao wawaache wapimane ubavu kidogo na walipotoka nje wakaachiwa ‘ulingo’ ndipo ngumi zilianza kupigwa.

Habari zaidi toka eneo la tukio zilisema kuwa: “Watu waliwazunguka huku wakishangilia kwa muda wa dakika tano ngumi zinapigwa ndipo maabaunsa wakawaamua, lakini, tayari TID alikuwa ameshatolewa manundu kadhaa puani.”

Aidha, kwa upande wa Babuu, alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, watu wa karibu na Babuu walilieleza kuwa, kufuatia TID kuchezea mkong’oto huo, kumezuka ‘bifu’ kubwa na kuna wasiwasi wa kutekana kwa mastaa hao hivyo huku Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba akitakiwa kuingilia kati suala hilo ili kuepusha

Chanzo cha umbea huu ni blogu ya XDeejayz.
 
TID nae kazidi jamani! Kha! Mara dudubaya, mara hasheem thabit! Inawezekana akawa mchokozi!
 
babuuu wa vichaa kawa na uso kama wa bibi kizee vinundu vya ngada na utozi wake wa kizamani,ubitoz nyangema,anajitutumua lakini hanogi tena tid nae siku izi sijui ata kama anaoga..kweli kila kitu kina mwisho.
 


hawa matoz njaa wamebaki kuchekesha tu mjini hapa...ila nachowakubali wanajitutumua hawakubali matokeo
 
"mastaa hao" kumbe bongo kuna star anaitwa babu? ngoja nirudi haraka inawezekana nakosa vingi.
 
babuu si dio yule wa king'oko mshikaji wake mtoto wa vasco da gama?
 
Hivi huyu ndo aliwahi kufungwa baadaye akaachiwa kwa huruma ya baba mwanaasha? Au nachanganya
Angekuwa wa kukoma angeshakoma siku nyiingi! wa mbili huyu, havai moja!
 
Aiseee jf kiboko/

babuuu wa vichaa kawa na uso kama wa bibi kizee vinundu vya ngada na utozi wake wa kizamani,ubitoz nyangema,anajitutumua lakini hanogi tena tid nae siku izi sijui ata kama anaoga..kweli kila kitu kina mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…