TID kutinga tena kituo cha kati cha polisi kivingine

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mwimbaji TID aka Mnyama kama anavyopenda kuitwa, ametishia kutinga katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Quick Rocka na kundi la OMG.

TID ambaye ana historia ya kufikishwa yeye kwenye kituo ha polisi na hata kufungwa miezi kadhaa, sasa amebadili upepo na yeye anahitaji haki yake kisheria.

Kupitia mtandao wa Instagram, Mnyama ametishia kufika polisi kuwasilisha malalamiko yake kutokana na kile alichodai kundi la OMG na Bosi wao Quick wametumia wimbo wake ‘Watasema’ bila ruhusa yake. Hivyo, anahitaji kulipwa angalau milioni 20 kama kifuta jasho kwa kazi yake iliyowahi kushinda tuzo mbili.

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK [HASHTAG]#Watasema[/HASHTAG], ameandia msanii huyo. Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.” ameandika TID.

‘Watasema’ ni hit ya miaka mingi iliyopita, ambapo TID alimshirikisha Naaziz, malkia wa michano kutoka Necessary Noise ya Kenya.

Chanzo: Mpekuzi
 
Alosto imemkaba iyo milioni ishirini yote atanunulia poda
 
Wamlipe tu hakuna namna, akili za kukaa kwa bi mkubwa hizo
 
Mkuu we mbona mbishi Khaleed ameshasema hilo jina la TID alitaki anataka kuitwa Khaleed au Mnyama hilo jina la TID tuwaachie watu wa mikoani
 
hivi central police maana yake kituo cha kati? nani mwazilishi wa hii tafsiri sisisi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…