Tidjane Thiam aukana Uraia wa Ufaransa ili kugombea Urais wa Ivory Coast

Tidjane Thiam aukana Uraia wa Ufaransa ili kugombea Urais wa Ivory Coast

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Credit Suisse, Tidjane Thiam ,62, ameukana uraia wake wa Ufaransa ili kutimiza masharti ya kushiriki katika uchaguzi wa urais wa Ivory Coast unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
IMG_3026.jpeg

Mwaka 2023, Thiam alichaguliwa kuwa kiongozi wa PDCI moja ya vyama vikuu vya upinzani huko nchini Ivory Coast na kumfanya kuwa mgombea wake.

Soma: Rais wa Ivory Coast awafukuza wanajeshi wa Ufaransa nchini Ivory Coast

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook, Thiam amesema amewasilisha ombi la kurudisha hati yake ya kusafiria ya Ufaransa, ili kubaki kuwa raia wa Ivory Coast.
 
Anaijua Afrika vizuri?asije akadhani huko mambo ni mepesi kwa sababu amesoma
 
Una shida gani?
Unahisi nchi kama Japan, Misri, China, Iran, Morocco, Ufaransa, Uturuki, Urusi unaweza kuwa raia wa nchi nyingine alafu ghafla ukane uraia huo na kugombea kati ya nchi hizo?

Huo ni kama uwendawazimu. Yaani kwa maslahi uliona uwe na uraia wa nchi nyingine, maslahi yakaisha ukastaafu hiyo nchi sasa unakana uraia wake unaenda kugombea nchi yako ya zamani kutafuta maslahi. Mapandikizi haya
 
Kwa mabara mengine kunaweza kuwa tofauti kidogo, kwa Africa nchi zimeuzwa na wazawa kabisa hivyo, hakuna tofauti ya mzawa na mtu mwenye uraia pacha.
 
Ni kweli atakuwa na uchungu na ivory coast, usikute hilo ni pandikizi la wafaransa
 
Back
Top Bottom