Tido Mhando Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari

Tido Mhando Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Snapinsta.app_460377230_3985706428419613_1410036865296467898_n_1080.jpg
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amemteua Tido Mhando kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa wizara hiyo, Isabela Maria Katondo imeeleza kuwa wajumbe wa Bodi hiyo Thobias Makoba, Mgaya Kingoba, Dk. Rose Reuben, Dk. Egbert Mkoko na Ladislaus Komanya.

Bodi hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 11 cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari Na. 12 ya mwaka 2016.
 
Tido Mhando aliacha kazi Bbc london kuja kuijenga Tbc malipo yake yalikuwa ni kumbambika kesi.

Namshauri mzee Tido Mhando achana na hawa wahuni wa ccm wanataka kukuchafuwa tena, pumzika kula pensheni yako.
 
Wingine hatuna tatizo tukiona Majina ya Wenyewe hatulalamiki ndio kawaida
Tunasema tuko pmj
 
Tido Mhando aliacha kazi Bbc london kuja kuijenga Tbc malipo yake yalikuwa ni kumbambika kesi.

Namshauri mzee Tido Mhando achana na hawa wahuni wa ccm kukuchafuwa tena, pumzika kula pensheni yako.
Mkuu, Hawa watu walifikiri akija nchini atajitoa ufahamu. Wakaona jamaa kichwa amedhamilia kuleta mageuzi ya kweli, na wao hawayahitaji.
 
Tido ni jembe aliibadilisha sana TBC kipindi kile wakamuona hafai akala shavu Azam akafanya mapinduzi mpaka Leo tunaona na ligikuu ya kwetu,wakiweka siasa pembeni professionalism isimame atakuwa MTU sahihi
 
Mkuu, Hawa watu walifikiri akija nchini atajitoa ufahamu. Wakaona jamaa kichwa amedhamilia kuleta mageuzi ya kweli, na wao hawayahitaji.
Mdahalo kwa wagombea ubunge mchakato majimboni ndio ilimuondowa, Makamba akaona wagombea vilaza wa ccm wanavyoumbuka na kipindi kikasitishwa akabambikwa na kesi juu.

Huyu mlevi Ayoub Ryoba ndio watu inaowataka ccm kutangaza mafanikio na kishindo cha awamu ya 6.
 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amemteua Tido Mhando kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa wizara hiyo, Isabela Maria Katondo imeeleza kuwa wajumbe wa Bodi hiyo Thobias Makoba, Mgaya Kingoba, Dk. Rose Reuben, Dk. Egbert Mkoko na Ladislaus Komanya.

Bodi hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 11 cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari Na. 12 ya mwaka 2016.

Ukichunguza kwa umakini Sana kuhusiana na madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo ya Waandishi wa Habari hasa ni Serikali kutaka kuwadhibiti Waandishi wa Habari ili kusudi Waandishi wote kabisa wawe Machawa na Waimba Mapambio ya Kusifu na Kuabudu Watawala pamoja na Vibaraka wao. Nothing good!

Waandishi wa Habari watakaokataa Kusifu na Kuwaabudu Watawala na Vibaraka wao basi watakumbana na Visa na majanga ya Kufungiwa Leseni zao, Kunyang'anywa pamoja na Kufutiwa Usajili wa kufanya kazi za Uandishi wa Habari hapa Tanzania.

Kwa hiyo Waandishi wa Habari wajiandae Kisaikolojia kukabiliana na janga hili jipya linalowanyemelea.
Wakumbuke kisa Cha Fatma Karume kufungiwa Leseni ya Uwakili hapa Tanganyika.

Waandishi wa Habari wa Tanzania sasa watakuwa na kazi moja tu ya :
Kusifu na Kuabudu Watawala!
 
Back
Top Bottom