Tigo inavyowafanyia watumishi wake sio haki

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Ikiwa ni siku chache tu toka tuuanze mwaka wafanyakazi wa Tigo wapatao 110 wameuanza mwaka vibaya ni wale waliokuwa wanafanya kazi tigo katika ofisi iliyokuwepo Quality Center pugu road waliokuwa wanajulikana kama Outbond Sales Agents.

Watumisi hao walidanganywa yakuwa ofisi ile haitaendeshwa tena na tigo hivyo inapewa mzabuni ajulikanaye kama PCCI hivyo baada ya sikukuu za Xmas na mwaka mpya wataanza kazi chini ya PCCI kwa kusaini mikataba mipya lakini haikuwa hivyo kwani PCCI iliwachukua watumishi 30 tu na kuwaacha hao wengine.

Imagine mkataba unavunjwa bila utaratibu wowote tena kijanjajanja bila ya huruma na kutambua kuwa kuna vijana walio na familia kutokana na kazi ile inakuja tu ghafla mtu anasimamishwa bila procedure zozote tena ghafla.

Nimewashauri watumishi hao waende mahakamani wakafate haki zao kwani haiwezekani uachishwe kazi ghafla tu bila hatua zozote tena kwa kudanganywa unahamishiwa kwingine.

Mkasa namba mbili ni wa kuchekesha sana PCCI wanyonyaji wakubwa sana kwa wale 30 waliochukuliwa wamepewa mikataba mipya na ya kinyonyaji;
-Kufanya kazi zaidi ya masaa kumi kwa siku
-No over time
-Gross salary 400K per month
-Take home 200K per month

Hii sio haki hata kidogo!
Tumekuwa tukiipenda na kuithamini Tigo ila kwa haya mnayowafanyia wadogo zetu tutakutana mahakamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duuh
sababu hasa ya kufanya hivyo ni nini?
 
Si kama walivyowafanyia wa call center!

Viongozi wamejikalia kimya!
 
Hizi outsourcing kampani ni shida tupu kiongozi! nawakumbuka sana Ero link walivyonyanyasa vijana
 
Hii kampuni yenu pendwa ina majanga kweli kila jina baya pia hupewa wao
 
Hakuna kesi rahisi kushinda kama hii.. nendeni mahakamani kwa umoja asiende mmoja.
Ikiwa ni siku chache tu toka tuuanze mwaka wafanyakazi wa Tigo wapatao 110 wameuanza mwaka vibaya ni wale waliokuwa wanafanya kazi tigo katika ofisi iliyokuwepo Quality Center pugu road waliokuwa wanajulikana kama Outbond Sales Agents.

Watumisi hao walidanganywa yakuwa ofisi ile haitaendeshwa tena na tigo hivyo inapewa mzabuni ajulikanaye kama PCCI hivyo baada ya sikukuu za Xmas na mwaka mpya wataanza kazi chini ya PCCI kwa kusaini mikataba mipya lakini haikuwa hivyo kwani PCCI iliwachukua watumishi 30 tu na kuwaacha hao wengine.

Imagine mkataba unavunjwa bila utaratibu wowote tena kijanjajanja bila ya huruma na kutambua kuwa kuna vijana walio na familia kutokana na kazi ile inakuja tu ghafla mtu anasimamishwa bila procedure zozote tena ghafla.

Nimewashauri watumishi hao waende mahakamani wakafate haki zao kwani haiwezekani uachishwe kazi ghafla tu bila hatua zozote tena kwa kudanganywa unahamishiwa kwingine.

Mkasa namba mbili ni wa kuchekesha sana PCCI wanyonyaji wakubwa sana kwa wale 30 waliochukuliwa wamepewa mikataba mipya na ya kinyonyaji;
-Kufanya kazi zaidi ya masaa kumi kwa siku
-No over time
-Gross salary 400K per month
-Take home 200K per month

Hii sio haki hata kidogo!
Tumekuwa tukiipenda na kuithamini Tigo ila kwa haya mnayowafanyia wadogo zetu tutakutana mahakamani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kima cha chini cha serekali ngazi ya mshahar in 150000 hivyo sio mbaya

Kula raia apambane na hali yake watumishi was umma walivyokaliwa kooni mlifurahi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom