Nilikuwa Facebook, nikaona swali kwenye matangazo pembeni, nikalijibu, wakaniambia nimeshinda sms 100, ninachotakiwa kukifanya ni kuweka simu no. yangu, wakanipa kodi nikatia kwenye simu yangu. Wiki 1 imenila euro 15. kila wakati napata sms ambayo inachukua kama 2.50 euros. Nikaenda ofisi yao , wakasema lazima uende online ku-cancel. Nikienda online , kuna fomu wanataka details zangu zote, nami naogopa kuwapa , maana wanaweza kuzitumia kutengeneza contract,maana mimi sija omba huduma ya vitu wanavyonitumia(mms,nyimbo ku-download, nk) Sina njia nyingine , inabidi kubadili no. ya simu. Never again nimekoma!