Tigo, nini umuhimu wa hii huduma ya "Longa Nae"?

Tigo, nini umuhimu wa hii huduma ya "Longa Nae"?

Babeli

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2015
Posts
6,702
Reaction score
3,272
JF,

Naomba kujadili Hawa jamaa wa TiGO Nini hii Longanae, utakuta nusu ya airtime ambayo unalipia mfano kwa Sh 3,000 kifurushi Cha Combo kwa wiki unapata muda wa maongezi dakika 200.

Kati ya hizo dakika 100 wanazi-fix automatic kwa mtu mmoja tu unayemchangua kuongea nae muda mrefu na dk 100 zinazobaki ndio wanakuachia uongee na mitandao yote mingine.

Sasa naona hii sio sawa, it's not fair at all msitulazimishe biashara ambayo ni vikwazo kwa wananchi embu jaribuni kuwa fair...huyo Longanae Ana I muhimu kiasi hicho Cha kumpa 50% ya gharama ya kifurushi kweli?

Sio sawa, hata basi mngeweka 10% tu, ili watumiaji tuwe na wigo mpana wa kutumia vifurushi vyetu..wananchi kwa Mpango huu tunahisi kuibiwa kwa sababu mwisho wa siku muda wa kifurushi unaisha unakuta sehemu ya Longanae Wala hujaimaliza.

Narudia it's unfair business msingoje mpaka wananchi wakaanza kupiga kelele bila sababu watu wa TiGO mnasikia?

TCRA

Minister of communication
 
Mi naomba maana ya haya maneno, (my)(wangu), wanaposema my wangu wanamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom