Tigo, ofa yenu ya MB za Boomplay inakera

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Hii ofa kiukweli haina maana kwa baadhi yetu, maana unaangalia salio linakuja sms refu la ma MB ya kusikiliza nyimbo Boomplay.

Yaani hapo unakuta una MB 200 za kuperuzi mtandao wowote lakini una GB 10 za kusikiliza nyimbo Boomplay, wakati sisi baadhi yetu siyo wapenzi wa kusikiliza nyimbo kwenye hiyo digital platform.

Kama mmeamua kutoa ofa ya MB toeni pasipo kum-limit mtumiaji kwamba azitumie kwa kitu gani.

Ni bora unipe hata ofa ya MB 10 za kuperuzi mtandao wowote kuliko unipe MB 700 kisha unanipangia nizitumie wapi.

Hii ofa yenu haina maana.
 
halafu wana matangazo kibao kama ya betting company! pumbafu sana hawa wanafanya mtandao ubakie wa wanafunzi
 
Inaweza ikawa haina maana kwako sasa Na sisi tunatumia simu za torch tuseme mb hazina maana ,Au mm simu yangu haina button niseme sms hazina maana ? Nunua bundle kulingana Na matumizi yako unayoyatumia acha kulalamika
 
Nilidhani mimi peke yangu, hadi nimeacha kununua MB za Tigo nimerudi Vodacom
 
Hii ofa kiukweli haina maana kwa baadhi yetu, maana unaangalia salio linakuja sms refu la ma MB ya kusikiliza nyimbo Boomplay.

Yaani hapo unakuta una MB 200 za kuperuzi mtandao wowote lakini una GB 10 za kusikiliza nyimbo Boomplay, wakati sisi baadhi yetu siyo wapenzi wa kusikiliza nyimbo kwenye hiyo digital platform.

Kama mmeamua kutoa ofa ya MB toeni pasipo kum-limit mtumiaji kwamba azitumie kwa kitu gani.

Ni bora unipe hata ofa ya MB 10 za kuperuzi mtandao wowote kuliko unipe MB 700 kisha unanipangia nizitumie wapi.

Hii ofa yenu haina maana.
Kwanza ni waongooo. Kuna siku niliingia boomplay kusurf na hizo mb zao nikijua zinaenda za boomplay nakuja kushtuka wamekula mb 200 zangu af za boomplay ziko pale pale
 
Back
Top Bottom