TIGO-PESA; Wezi au Matapeli?

TIGO-PESA; Wezi au Matapeli?

eedoh05

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
632
Reaction score
235
Tigo ni miongoni mwa kampuni kubwa za simu hapa nchini tangu enzi za "mobitel" "buzz" na sasa tigo. Ila kwa sasa wamekuwa walaghai/ waongo/ wajanja/ wezi?....... sijui ni waweke kundi gani?

Ni muda mfupi tigo kupitia huduma yao ya TIGO-PESA kwamba unapotuma pesa kwa tigo-pesa kwa kiwango cha elfu kumi na chini yake atalipia au atatozwa shilingi 50 za kitanzania kwa huduma hiyo. Lakini SIVYO WAFANYAVYO! Ukituma kati ya Tsh 1,000 hadi 10,000/- wanatoza sh. 550/-. Je huo sio wizi/ utapeli.

NAOMBA KUWASILISHA!
 
Hao jamaa hawafai kwa wizi wa reja reja!
 
tigo ni miongoni mwa kampuni kubwa za simu hapa nchini tangu enzi za "mobitel" "buzz" na sasa tigo. Ila kwa sasa wamekuwa walaghai/ waongo/ wajanja/ wezi?....... Sijui ni waweke kundi gani?

Ni muda mfupi tigo kupitia huduma yao ya tigo-pesa kwamba unapotuma pesa kwa tigo-pesa kwa kiwango cha elfu kumi na chini yake atalipia au atatozwa shilingi 50 za kitanzania kwa huduma hiyo. Lakini sivyo wafanyavyo! Ukituma kati ya tsh 1,000 hadi 10,000/- wanatoza sh. 550/-. Je huo sio wizi/ utapeli.

Naomba kuwasilisha!

huduma zao usithubutu kuzijaribu,
1. Nilinunua umeme wa elfu10 mpaka leo sjawai kuupata walizama nao umeme nilikosa na ela walinikata mpaka leo hakuna majibu,
2. Vijana wao katika kujiongezea vipato wameamua kujiiinvolve katika kuwa swap watu na kuwasajili vibaka wenzao basi hapo wanapiga ela za watu si kawaida wahusika wakubwa, (dawa yao tunzeni password zenu ingawa wao c ndo wanaziifadhi izo passwords)
nami nawasilisha wizi unaofanywa na tigo
 
Nilikuwa na mpango wa kujiunga na tigo pesa bora umenijuza mapema nimeahairisha
 
Mimi walilazimisha wenyewe kuniunganisha kwa sababu kuna business tulifanya wakanambia wananilipa kwa Tigo pesa nilichokiona najua mwenyewe, wizi mtupu. Charges zao za kodraw pesa ndo utachoka. Unafuu wao uko kwenye kupiga cm togo to tigo basi.
 
wanakata ela nying sana wakat wakudraw, napata was was sana na hii huduma yao japo iko fast bt too costful
 
Mimi nilinunua umeme wa sh 15000 kwa tigo pesa wiki 2 zilizopita mpaka leo sijapata huo umeme na hela walinikata. Sina hamu na hiyo huduma ni wizi mtupu!
 
Nakubali makato ni makubwa sana kutuma na kupokea pesa tofauti na washindani wenzao. Umeme nanunua kwa Tigo Pesa siku zote, LUKU na sijawahi kuwa na tatizo, ni chap chap natumiwa nambari za kuingiza kwenye mita yangu ya Luku.
 
Yote haya yanatakiwa kudhibitiwa na TCRA je wana habari na haya? Halafu inakuwaje ukituma pesa uchajiwe na yule anayetumiwa naye alipe wakati akichukua? Tunahitaji ufafanuzi kama sio wizi ni nini?
 
Kwakweli mimi mpaka leo nina wasiwasi na hizi huduma za pesa kwenye simu. mpaka leo sijajiunga kwa mtandao wowote ule
 
TCRA wako busy na kampeni za digitali wakati kuna mambo serious ya uwizi....
 
Back
Top Bottom