Tigo, Tanesco wezi tu

Tigo, Tanesco wezi tu

Kichuchunge

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
384
Reaction score
970
Niende moja kwa moja kwenye mada. Jana nilinunua umeme kwa kupitia simu yangu ya mkononi. Sikujua kuwa kulikuwa na tatizo la kimtandao katika mojawapo ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo au Tanesco wanaouza umeme.
Kibaya zaidi, baada ya kununua umeme, pesa ilikatwa kwenye Tigopesa lakini hakuna ujumbe wowote uliorudi kwangu, si kuletwa Token, kutaarifiwa kama kuna tatizo wala kurudishiwa pesa yangu. Nilisubiri kwa muda mrefu kuokama watanirushia pesa yangu lakini wapi. Sijaona chochote mpaka leo. Sijajua ni nani mwenye tatizo, Tanesco au Tigo. Kama ni wote basi huu ni wizi wa kutisha. Unadhani kwa siku moja wakichukuliwa watu sh 10,000 kila mmoja kwa nchi nzima zitapigwa sh ngapi? Nirudishieni pesa zangu. HUU NI WIZI!
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa chagamoto hiyo, tunapenda kufahamu ka ulifanikiwa kupata token za umeme ulionunua tafadhali.^OK
 
Back
Top Bottom