Tigo, Vodacom wakubaliana usafirishaji fedha

Tigo, Vodacom wakubaliana usafirishaji fedha

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Kampuni za simu za mkononi Tigo na Vodacom zimeungana pamoja katika utoaji wa huduma za fedha kwa njia ya mitandao ambapo kwa sasa wateja wa kampuni hizo watanufaika na huduma za upokeaji na uwekaji wa fedha.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo Meneja Mkuu wa Tigo Diego Guiterrez alisema wateja wa Tigo wanaweza kutuma fedha kwenda Vodacom kwa tozo la kiwango kilekile kinachotozwa kwenda Tigo.

"Lengo ni kuhakikisha kuwa tunawapatia huduma bora wateja wetu wanaotuma fedha kwenda Vodacom na hii imekuja ikiwa ni baada ya kuungana na Airtel na Zantel mwaka jana," alisema Guiterrez.

Alisema kuwa wateja wa Tigo wanaweza kutuma na kupokea fedha kati ya Tigo Pesa na Tigo Cash Rwanda yenye uwezo wa kubadilisha aina ya ankara moja kwa moja.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Rene Meza alisema kuwa ushirikiano huo pia ni fursa kwa wateja wake kujiongezea wigo wa ufanyaji wa shughuli mbalimbali zinazohusisha utumaji wa fedha kwa njia ya simu katika ufanyaji wa biashara.


Chanzo: Habari leo
 
Wafanye usafirishaji na kwa mawakalanahisi itakuwa ghali.
mwisho wa siku mlaji ndo anaingia garama kubwa kusafirisha cost vs benefits = Benefits > costs
 
Back
Top Bottom