tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

Soma Pia:

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
 
KESI NI NGUMU SANA HII KWA UPANDE WA LISSU.

Tatizo linapokuja ni kwamba walioshitakiwa ni Millicom sio Tigo (Nimeatanisha attachments)

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama inayomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Kuanzia mwaka 2022 kampuni mama mpya ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Honora wataendelea kujibanza kwenye angle ya kumshinikiza Lissu aendelee kuwashtaki Millicom aliowafungulia kesi.inavyoonekana Millicom walivyoona ngoma inakaribia kupasuka wakaondoka mwaka 2022

Lissu ilibidi awashtaki Tigo kwasababu hata kampuni mama ikibadilika angeendelea kuwashtaki Tigo.
 

Attachments

huu mtama au ngwara..?

Inayoshtakiwa ni Kampuni siô Mmiliki.
Hivyo Kesi bado Ipo palepale.

Nilitegemea Wakanushe kuwa hawakufanya hivyo lakini Kwa kauli yao inathibitisha kuwa kitendo kilifanyika na kilifanywa na Kampuni ya Tigo, semà Mmiliki ni Mwingine.

Jina la Kampuni NI lilelile.
Wateja wa Tigo na Namba za tigo ni zilezile ikiwemo Mhanga àmbaye ni Tundu Lisu

Hivyo Kesi Hapo bado yamoto.
 
Back
Top Bottom