Tigo wamemzuia msanii Mwana FA kuingia Fiesta Arusha

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Watu wanaojulikana kutoka kampuni ya Tigo usiku wa jana wamkataza mwana FA kuingia katika shoo ya Tigo fiesta kama mtazamaji wa kawaida sababu anaidai kampuni hiyo bil 2.5.

Wataalam wa sheria hii imekaaje?

========
FULL STORY
========

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo ni mdhamini mkuu wa tamasha la Fiesta mwaka huu lililobatizwa jina la ‘Tigo Fiesta’ linaloandaliwa na Clouds Media Group, imedaiwa kuwazuia Mwana FA na AY kushiriki tamasha hilo.

Kwa mujibu wa wasanii hao, kampuni hiyo sio tu kwamba imewazuia kutumbuiza bali pia wamezuiwa kuhudhuria kwenye tamasha hilo kama mashabiki na nyimbo zao zimepigwa marufuku.

Mkali huyo wa ‘Dume Suruali’ ameripotiwa kuzuiwa getini alipojaribu kuingia kwenye tamasha hilo lililofanyika jana jijini Arusha ambapo alienda kama shabiki wa kawaida.

FA ametoa ujumbe huo akiwa ameuweka katika hali ya kejeli na mshangao akihoji uhalali wa marufuku ya kampuni hiyo ambayo walisigana nayo mahakamani hivi karibuni wakiidai zaidi ya shilingi bilioni 2 na kuishinda.




Kwa upande wa AY, alikumbushia zuio la nyimbo zao kupigwa kwenye tamasha hilo ambalo lilidhaminiwa pia na Tigo.

Hivi karibuni, Mahakama Kuu ilibariki uamuzi wa Mahakama ya Wilaya wa kuitaka kampuni hiyo kuwalipa AY na FA kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2 baada ya kujiridhisha kuwa walitumia nyimbo zao mbili kama miito ya simu bila idhini yao. Kesi hiyo ilidumu kwa takribani miaka mitano.

Mwanasheria wa wasanii hao, Alberto Msando amesema kuwa kitendo cha kuwazuia wasanii hao kuingia kwenye tamasha hilo ni cha kitoto na cha ajabu.




Dar 24
 
Nina sherehe yangu ukumbi nimelipia kila kitu nawe unajisogeza nakukataza kuweka nguvu wako. Unaweza kwenda polisi kushitaki!?
 
kampa, kampa tena 😀😀
 
Mambo ya Lugumi na Sirikali haya. TehTeh.
 
Hata Ulaya kuna baadhi ya mashabiki wa soka huwa inatokea wanapigwa marufuku kuingia viwanjani licha ya kuwa na fedha za kiingilio.
 
Duuh wanatia aibu Sana
 
Walitaka vijana wa watu wasidai haki zao?

Mimi nasema wasonge mbele, wasilegeze kamba..

Wasanii wengi wanaogopa kupigania haki zao hasa kwenye media hizi kwaajili ya upumbavu kama huo!
 
Dawa ya deni kulipa sio kumzuia kuingia ukumbini....


Walipe tu hakuna namna
 
Reactions: BAK
Hao tigo nao mbona hela ndogo sana hiyo kwao? Wanheamua tu kupatana pembeni wangewapiga hata milioni 500 kama za Idrisa wa bigbrother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…