Tigo wameondoa makato ya shilingi 100 kimya kimya kwenye huduma ya NMB Mobile

Tigo wameondoa makato ya shilingi 100 kimya kimya kwenye huduma ya NMB Mobile

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Kilichoniondoaga voda ni hii ishu ya sh.100 sasa nilivyokuja tigo nao haikuchukua muda wakaanzisha huo ujinga tena bila kuarifiwa wala kushirikishwa.

Mshahara jana ukaingia kwa wengine na ukachelewa kwa baadhi yetu basi watu kutokana na kupigika wakawa wanachungulia moja kwa moja accounts zao.

Binafsi sikuwa na wazo la kuangalia kutokana na kwamba sikuwa na salio (vocha) kwenye simu yangu (wenzangu halotel - bure). Ajabu leo DED kafanya mambo nikaanza kufanya matumizi ndo nashangaa siambiwi tena kwamba nicomfirm kukatwa 100.

Nikasema labda nimekosea nikacancel kisha nikaingia upya bado naona mwendo mtelezo baasi nikasema tigo kwisha jeuri yake. Wanamind vitu vidogovidogo mpaka wanajishtukia ona sasa wanajirekebisha kwa aibu kimyakimya. Japo nisishangilie sana maana najua tu badala tumeachiwa huku lazima kuna sehemu nyingine tunaenda kupigwa zaidi.

Mtu asije kunidis kwa uzi huu kwasababu kwangu mimi hili ni la kufurahia kabisa.

"Watanzania tunapenda/tumezoea vya bure."
 
Acha kujifanya una uelewa mkubwa..


Kwahiyo ukashindwa kuandika kuangalia salio NMB mobile kupitia USSD code?
Sina uelewa mkubwa hata (wala sijajinasibisha hivyo) ila nilichoandika nina uhakika kinaeleweka dhahiri shahiri na ndio maana uliporudia kusoma ukaelewa.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ulivyotiririka imependeza ni kama upo mahali unajipooza kwa maji ya shaba baridiiii
 
Back
Top Bottom