Ni kweli kabisa Tigo wamejali kipato cha watanzania walio wengi kwa sasa,lakini watadumu kwa muda gani katika hiyo nafuu?
Unajua hii mitandao ya kampuni za simu iko hivi katika gharama zake ambazo binafsi nilipata hesabu zake nikiwa na kampuni moja ambayo ilisimamisha/jenga transmission tower zote za Vodacom-TZ,mpaka mwaka 2006 kujenga tower 1 ilikuwa sio chini ya Tshs million 120,halafu maintenance ya tower 1@mwezi ni Tshs million 20.
Aina hii ya mawasiliano inaitwa peer to peer communication,hapa satellite dishes zinatumika pia;bado kuna gharama nyingine nyingi tu ktk kufanya kampuni ifikie malengo yake;hapa international calls zote zinapitia tena kwenye kampuni nyingine hii gharama nyingine hiyo;kwahiyo aina hii ya mawasiliano ni gharama sana kumilikiwa na kampuni moja ya simu pekee.
Ndiyo maana TCRA waliwakalisha chini makampuni yote ya simu kwa sharti la kupunguza gharama za simu hapa nchini;lakini,makampuni karibia yote yalikataa kwa kigezo cha gharama za uwekezaji hazijarudi bado.TCRA wakapendekeza kampuni zote zi-share miundombinu ya mawasiliano kwa pamoja ili kupunguza gharama za uendeshaji ili mtumiaji apate ahueni ktk tarriff charges,kufikia hapa kikao kikavunjika.
Lakini technolojia latest katika mawasiliano ya simu na mtandao/internet hivi sasa ni optic fibre,ambayo hii ndiyo the fastest uki-click tu page imekwisha funguka inakusubiri u-apply command nyingine.
Hivi sasa,SEACOM wanajenga mkonga wa mawasiliano hayo(optic fibre backbone) kutoka Cape town-South Africa kupitia Bahari ya Hindi hadi Malindi-Kenya.Na mradi huu unategemewa kukamilika June,2009.
Kukamilika kwa mradi huu kutaleta nafuu sana kwa watanzania katika mawasiliano ya simu na internet/mtandao kuliko hivi sasa,hili ndilo suluhisho la mawasiliano.