Tigo yawang’ang’ania MwanaFA, AY

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imekubali kusikiliza maombi ya kampuni ya Tigo, kuhusu fidia ya Sh2.1 bilioni ilizoamriwa kuwalipa wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinyijuma na Ambwene Yesaya.

Mahakama imekubali kusikiliza maombi ya kampuni hiyo baada ya kutupilia mbali pingamizi la awali lililowekwa na wasanii hao, Mwinyijuma maarufu MwanaFA na Yesaya maarufu AY.

Mahakama hiyo Aprili 11, 2016 iliiamuru Tigo kuwalipa fidia ya kiasi hicho cha fedha wasanii hao kwa kosa la kukiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, kwa kutumia kazi zao (nyimbo) kama miito ya simu bila ridhaa wala makubaliano nao.

Nyimbo hizo ni Usije mjini wa MwanaFA na Dakika moja wa AY. Kutokana na hukumu hiyo, wasanii hao walifungua maombi ya utekelezaji.

Hata hivyo, Tigo ilifungua maombi mahakamani hapo ikiiomba Mahakama iamuru kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, ijumuishwe kwenye hukumu kama mmoja wa wadaiwa kwa kuwa wanataka nayo ijibu hoja za wadai.

Wakili Rosan Mbwambo anayeiwakilisha Tigo, amesema mteja wake aliingia makubaliano na Cellulant iwapelekee nyimbo na hakujua kama kampuni hiyo haikuwa na makubaliano na wahusika.

Ingawa katika kesi ya msingi kampuni hiyo ilikuwa mmoja wa wadaiwa, lakini hukumu haikuwataja jambo ambalo Tigo katika maombi yake inadai iliachwa kwa bahati mbaya.

Wasanii hao kupitia wakili Albert Msando waliweka pingamizi kuhusu maombi ya Tigo, wakiiomba Mahakama iyatupilie mbali.

Walidai kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, kilichotumika kufungua maombi hakiiwezeshi Mahakama kutekeleza maombi hayo kwa sababu kosa la kutokuihusisha kampuni hiyo si la kiuandishi wala kihesabu.

Pia, walidai kama Tigo ilitaka kampuni hiyo iongezwe, ilipaswa kufungua maombi ya marejeo au kukata rufaa.

Akitoa uamuzi leo Jumatatu , Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo amesema hoja hizo hazipaswi kuwasilishwa kama pingamizi. Amesema zitasikilizwa wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo kama kampuni hiyo iliachwa kwa bahati mbaya au la.

Hakimu Tarimo amepanga kusikiliza maombi hayo Jumatano Oktoba 18.

Awali, Tigo ilifungua maombi Mahakama Kuu ikiomba kusimamisha utekelezaji wa hukumu.

Wasanii hao waliweka pingamizi na kushinda, ndipo walipofungua maombi ya utekelezaji wa hukumu hiyo.


Mwananchi
 
Ay/FA anzeni kuipangia matumizi hiyo hela mshaipata, ikiwezekana muanze kukopa Tigo watalipa
Kufungua kesi ya madai ni jambo jingine, kushinda kesi na kulipwa ni jambo jingine...

Ikitokea wameshindwa, tiGO wanaweza wakaiomba mahakama kutokulipa deni kwa mkupuo bali kwa vipindi tofauti tofauti kiasi kwamba wanaoweza kuja kufaidi ni wajukuu wa hao mabwana...
 
Inadakwa "bombadia" ya tigo fasta kinaeleweka.
 
Tigo ni matapeli kama matapeli wengine tu.
 
Tigo wanataka wao wasilipe hiyo hela bali kampuni iliyo leta hizo nyimbo kwa Tigo.
 
itachukua muda sana hadi hao watu kuja lipwa hizo hela
 
Tigo wanataka wao wasilipe hiyo hela bali kampuni iliyo leta hizo nyimbo kwa Tigo.
Mwisho wa siku watalipa tu mkuu,aliekutwa ngozi ndie alieua chui hii kanuni ina nguvu sana,popote pale duniani
Mtandao uliotumika kucheza hizo nyimbo ni wa Tigo na sio cellunet,kisheria Tigo wanatakiwa wawafungulie cellunet kesi kuwadai hiyo hasara na sio kuomba waingizwe kwenye hukumu
 
Kweli hawa wasanii nyimbo zenyewe zipi za kulipwa mapesa yote hayo,sana sana thamani ya nyimbo hizo haifiki hata laki ya kibongo
 
Nilijua wameshalipwa na zimeshaliwa na michwa. Kumbe bado wanadanadana ?!!!
 
Kweli hawa wasanii nyimbo zenyewe zipi za kulipwa mapesa yote hayo,sana sana thamani ya nyimbo hizo haifiki hata laki ya kibongo
Waambie maboss wako Kuwa liwake jua inyeshe mvua hiyo pesa watatoa
 
Hiyo kampuni iliyokuwa imeingia mkataba na tigo ya kuwaletea nyimbo ikijumuishwa basi tigo watakuwa wameruka hilo deni. ..sioni tena wasanii wetu wakilipwa hizo pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…