rashid2025
Member
- May 14, 2024
- 5
- 3
Habari Wana Jukwaa,
Mimi ni mhanga wa tatizo ambalo linahusisha TigoPesa MasterCard. Niliafanya muamala kwenda Alibaba kwa ajili ya manunuzi. Mara ya kwanza nilifaulu kununua bidhaa bila matatizo. Baada ya mwezi mmoja, niliweka tena pesa kwenye TigoPesa na kufanya muamala wa pili tarehe 13.06.2024.
Hata hivyo, pesa haikufika. Nilipowasiliana na Tigo, walisema kuwa muamala umefanyika. Nilipowasiliana na Alibaba, walisema kuwa muamala haujafanikiwa na kama pesa imekatwa, niwasiliane na mtoa huduma ili pesa irudi.
Nilirudi tena kwa Tigo ambao walinipa masaa 72 kushughulikia muamala huo. Leo ni siku ya 17 na bado wanashughulikia muamala. Niliwasiliana na Dawati la Malalamiko la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuwapa maelezo yote. Baada ya siku mbili, walinitumia barua pepe kwamba walishawaambia wahusika watatue suala hili haraka.
Leo nimeingia kwenye app ya TigoPesa kuangalia kadi yangu na kugundua kuwa wameisitisha kadi.
Naomba ushauri wenu wanajukwaa maana dola 35 ni nyingi mno kwangu.
Je, inawezekana kuwaburuza mahakamani? Maana wahanga wa tatizo hili ni wengi.
Tafadhali niambieni taratibu za kufuata na nipeni ushauri wenu.
Asanteni.