Kila kitu kina gharama yake wapendwa.
Kabla hujafanya maamuzi jipime kama utamudu.
Hakuna jambo lolote lisilo na wajibu.
Kabla hujaamua kuolewa/kuoa jipime kwanza Kama utaweza au japo kujitahidi tu kuwa mke/mume.
Kabla hujaamua kuanzisha biashara jipime kama uko tayari kukabili changamoto zake.
Kabla hjaamua kuzaa jipime kama unaweza kulea.na kuwa mzazi bora.
Kabla hujajikita kwenye kilimo fikiria kuhusu utunzaji wa shamba,palizi na mbolea.
Wengi tunatamani kupata mafanikio maishani,lakini hatutaki kusulubika... matokeo yake tunaangukia za uso na kuanza kuroga au kwenye maombi na maombezi.
Imeandikwa utavuna ulichopanda.