Tik tok na X zafungwa nchini DRC

Tik tok na X zafungwa nchini DRC

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Msemaji mkuu wa serikali ya DRC, Patrick Muyaya, ametangaza kusitishwa kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya X na Tik Tok, kwa alichokiita kuepuka usambazaji wa taarifa za uongo, zinazopotosha raia na kuwaweka katika hali ya sintofahamu.
Zaidi, google play na yenyewe imezuiliwa ili watu wasiweze kupakua VPN.
Waziri wa mambo ya ndani alipoulizwa, alisema tu ni matatizo ya kiufundi yanayoshughulikiwa, na kwamba punde tu wataalamu watakapoweka mambo sawa, watu wataendelea kutumia.

Watu wengi wameonekana kulalamikia uamuzi huo na kudai ni ukikukwaji wa haki inayolindwa na katika ya DRC, kifungu cha 23 na cha 24.
 
Nchi nzima hakosekani aliyepakua VPN, wanarushiana kwa Xshare
 
Nchi nzima hakosekani aliyepakua VPN, wanarushiana kwa Xshare
sana tu. Amesahau kuwa huko Goma wanatumia mtandao wa Rwanda, wao hawana shida. Kuwasilisha kinachoendelea kwingine mbona simpo tu. Hata wakitumiana kwa email watainstall tu.
 
sana tu. Amesahau kuwa huko Goma wanatumia mtandao wa Rwanda, wao hawana shida. Kuwasilisha kinachoendelea kwingine mbona simpo tu. Hata wakitumiana kwa email watainstall tu.
Umeongeza la email 👍
 
Back
Top Bottom