Tiketi ya Man U UCL mikononi mwa Ajax

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Manchester United aka Mashetani Wekundu ya Uingereza wakicheza nyumbani OT jana wameweka miadi na Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa fainali ya kombe la Europa.

Man U ilitoa sare ya 1-1 na Celta Vigo ya Hispania jana na hivyo kushinda kwa 2-1 katika jumla ya mechi mbili. Nayo Ajax ilipata kipigo cha 3-1 toka kwa Lyon ya Ufaransa ingawa imetinga fainali kwa jumla ya mabao 5-4.

Kwakuwa bingwa wa Europa anapata tiketi ya makundi ya Klabu Bingwa Ulaya,ni dhahiri tiketi ya Man U iko mikononi mwa Ajax. Kwasasa Man U wapo nafasi ya sita katika Ligi Kuu ya Uingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…