Tiketi za kombe la dunia zaanza kugombewa

Tiketi za kombe la dunia zaanza kugombewa

ishuguy

Member
Joined
Nov 3, 2007
Posts
76
Reaction score
10
Patashika ya kununua tiketi za kuona mechi za kombe la dunia 2010 imepamba moto, siku chache baada ya droo ya michuano hiyo kufanyika Afrika Kusini.
Zaidi ya tiketi mpya milioni moja zimeingia sokoni, baada ya timu 32 kujulikana zitacheza na nani na kiwanja gani.
Mashabiki watatakiwa kuwasilisha maombi ifikapo Januari 22, kupitia wavuti ya Fifa na vyama vya soka vya taifa.
Mojawapo ya mechi zinazotarajiwa na mashabiki wengi ni ile itakayochezwa Juni 12, kati ya England na Marekani - mataifa hayo mawili yalinunua idadi kubwa ya tiketi katika michuano iliyopita.



Hivi wale wenzangu na mie tulifungua akaunti ya kudunduliza pesa kwaajili ya kwenda kwenye world cup S.A tufanikiwa kuzipata hizo tiketi kweli??
 
Back
Top Bottom