TikTok inajipanga kuzima huduma ya App yake kwa watumiaji wa Marekani kuanzia Jumapili hii ya Januari 19, iwapo Mahakama ya Juu haitazuia marufuku hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya The Information.
Muktadha: Kulingana na watu walioko karibu na suala hilo, hata wale ambao tayari wamepakua App hiyo hawataweza kuendelea kuitumia. Badala yake, watumiaji wataona ujumbe wa 'pop-up' unaowaelekeza kuhusu marufuku hiyo.
Wamarekani wengi wameanza kuhamia mtandao mwingine wa China Xionghongshu (Red Note)
Kupitia Red Note Wamarekani wameanza kuengage na Wachina na wameanza kugundua kuwa habari nyingi walizokuwa wanazipata kupitia media za Marekani ni propaganda wameanza kujionea hali halisi ya China