Watoto ambao ni wakimbizi huko Syria wamekuwa wakitengeneza videos ambazo wanaziweka Tiktok kisha watu wanaweza kuwatumia vitu vinaitwa diamonds ambavyo wanaweza kuvibadili kuwa pesa na kuitoa. Lakini, Tiktok huchukua 70% ya hizo donations na pia agent ambapo wanaenda kutoa pesa nao wanawakata pesa.
Mwandishi wa habari wa Aljazeera alijaribu kumtumia diamonds mkimbizi zenye thamank ya $106, lakini mpaka anachukua hiyo pesa kwa agent aliambulia $19 tu.
Walipoulizwa Tiktok kuhusu hilo, walijibu kuwa maudhui hayo hayaruhusiwi kwenye platform yao ndio maana wanaya discourage.