TikTok yaipiku Google kwa wingi wa watumiaji wa mitandao

TikTok yaipiku Google kwa wingi wa watumiaji wa mitandao

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
TikTok inapendwa zaidi na watumiaji mtandaoni kuliko Google ambayo imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 10 mtawalia.

Mtandao huo wa kushirikisha video unatembelewa zaidi kuliko Injini ya utaftaji ya Marekani, kulingana na Cloudflare, kampuni ya usalama IT.

Viwango hivyo vinaonyesha kuwa TikTok iliiondoa Google katika nafasi ya kwanza mnamo Februari, Machi na Juni mwaka huu, na imeshikilia nafasi ya kwanza tangu Agosti.

Mwaka jana Google ilikuwa ya kwanza, na tovuti kadhaa ikijumuisha TikTok, Amazon, Apple, Facebook, Microsoft na Netflix zote zilikuwa kwenye 10 bora.

Cloudfare ilisema inafuatilia data kwa kutumia zana yake Cloudflare Radar ambayo inafuatilia trafiki ya wavuti.
Inaaminika kuwa moja ya sababu za kuongezeka kwa umaarufu wa Tiktok ni kwa sababu ya janga la Corona, kwani marufuku ya kutotoka nje ilimaanisha watu walikuwa wamekwama nyumbani na wanatafuta burudani.

Kufukia Julai mwaka huu, App ya TikTok ilikuwa imepakuliwa zaidi ya mara bilioni tatu ,kulingana na kampuni ya data ya Sensor Tower.

Mtandao huo wa kijamii unaomilikiwa na kampuni ya China inayoitwa Bytedance, sasa ina zaidi ya watumiaji bilioni moja wanaofanya kazi kote duniani, na idadi hiyo inaendelea kukua.

Nchini China, ili kuzingatia sheria za udhibiti wa nchi, programu inaitwa Douyin, na inaendeshwa kwenye mtandao tofauti.

Douyin ilizinduli awali Septemba 2016. Mwaka huu, China iliamua kwamba watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 14 wangeruhusiwa kutumiaukuwaa hilo kwa dakika 40 kwa siku.

Hofu ya usalama
TikTok ilizinduliwa kimataifa mwaka wa 2018, baada ya kuunganishwa na huduma nyingine ya mitandao ya kijamii ya China, Musical.ly, programu ambayo iliwaruhusu watumiaji kushirikisha video zao za kusawazisha midomo (lip-synching) kwa nyimbo.

Mtando huo wa kijamii sio umekumbwa na utata mara kadhaa. Mnamo mwaka wa 2019, ilipigwa marufuku kwa muda nchini India, uchunguzi wa kijasusi wa Marekani ulibaini kuwa Musical.ly inaruhusu maudhui yaliyochapishwa na watumiaji wa umri wa chini na kutozwa faini ya pauni milioni 4.3 .

Kama moja ya App ya China iliyopata ufanisi mkubwa, wanasiasa na wadhibiti nje ya nchi hiyo wameibua wasiwasi kuhusu usalama na faragha.

Mwaka jana TikTok ililazimika kupinga madai kwamba inadhibitiwa na serikali ya China.

Theo Bertram, mkuu wa sera ya umma wa TikTok Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, alisema itakataa ombi lolote kutoka kwa China la kukabidhi data.

App hiyo ina shirikisha video fupi, zinazoangazia vichekesho, densi na siasa.
 
Hakika yaani hata YouTube wanajitahidi kua na features kama TikTok ndio maana wakaja na mfumo wa YouTube shorts.

Tik tok ina ma filter ya kufa mtu. Pia editing yake wameifanya easy sana. Ndio maana wapuuzi hasa wadada wa dunia nzima wameipenda sana
 
Tik tok ina ma filter ya kufa mtu. Pia editing yake wameifanya easy sana. Ndio maana wapuuzi hasa wadada wa dunia nzima wameipenda sana
kweli na hapa mitandao mingine ijipange kabisa maana ushindani wa TikTok utakuwa mkubwa.
 
Yani sijawahi tumia tik tok wala hata kuona app yake zaidi ya kukutana na video zenye logo ya tik tok.
Sijawahi kuwa na mzuka nayo
 
Different categories (Google being a search engine ) watu wanaweza kwenda sana huko kutafuta knowledge hayo mengine ni burudani tu...., hivyo ukizingatia wapenda burudani ni wengi kuliko wasaka knowledge it was just a matter of time....., Google wa maintain quality na kuendelea kukusanya information na kuzipackage vizuri mtumiaji wa google sio necessarily mtumiaji wa tik tok na vice versa
 
Wanaume wengi waliopo tiktok ni visamvu mchele.
Dah ila kumbuka kwa sasa TikTok ndio inazidi kuwa na watumiaji wengi hivyo wengine inawalazimu kuwa nayo ili waendelee kushika chart.
 
Yani sijawahi tumia tik tok wala hata kuona app yake zaidi ya kukutana na video zenye logo ya tik tok.
Sijawahi kuwa na mzuka nayo
Wapo wengi ambao hawatumii lakini kwa jinsi inavyo kuwa nahisi itajizolea watumiaji wengi.
 
Different categories (Google being a search engine ) watu wanaweza kwenda sana huko kutafuta knowledge hayo mengine ni burudani tu...., hivyo ukizingatia wapenda burudani ni wengi kuliko wasaka knowledge it was just a matter of time....., Google wa maintain quality na kuendelea kukusanya information na kuzipackage vizuri mtumiaji wa google sio necessarily mtumiaji wa tik tok na vice versa
Kweli licha ya TikTok kutrend kwa sasa lakini Google wamejiposition sehemu nzuri maana kila kitu utakitafuta.
 
Back
Top Bottom