TikTok yapewa muda hadi Januari 19, 2025 iwe imeuza hisa zake kwa mwekezaji wa Marekani au ifungiwe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama ya Rufaa ya D.C. imetangaza uamuzi wa kuunga mkono sheria inayotaka ByteDance, kampuni mama ya TikTok kutoka China, kuuza hisa zake za programu hiyo ifikapo Januari 19, 2025, la sivyo itakabiliwa na marufuku kote Marekani.
IMG_1309.jpeg

Sheria hiyo, inayojulikana kama Protecting Americans from Foreign Adversary Controlled Applications Act, imeelezwa kuwa imelenga moja kwa moja kulinda usalama wa taifa.

Hata hivyo, TikTok imepinga hatua hiyo, ikidai inakiuka haki ya Kifungu cha Kwanza cha Katiba ya Marekani (First Amendment).

Mahakama, kwa upande wake, imesisitiza kuwa ushahidi wa serikali ya Marekani kuhusu hatari za kiusalama una uzito mkubwa, ikizingatia ushawishi wa programu hiyo duniani na uwezekano wa matumizi mabaya.

Soma, Pia: Bunge la Marekani lapitisha Muswada wa Sheria ya kuifungia TikTok
==
The U.S. Court of Appeals for the D.C. Circuit has upheld a law requiring TikTok's Chinese parent company, ByteDance, to sell its stake in the app by January 19, 2025, or face a nationwide ban.

The decision supports the Protecting Americans from Foreign Adversary Controlled Applications Act, which the court deemed narrowly tailored to address national security risks.

While TikTok argues the law infringes on First Amendment rights, the ruling emphasised the app's global reach and potential for misuse, citing the U.S. government's persuasive evidence.
 
View attachment 3171068

Mahakama, kwa upande wake, imesisitiza kuwa ushahidi wa serikali ya Marekani kuhusu hatari za kiusalama una uzito mkubwa, ikizingatia ushawishi wa programu hiyo duniani na uwezekano wa matumizi mabaya
Wakati wenzetu wanapigania USALAMA wa nchi yao. Hapa kwetu serikali inapambana kudukua mawasiliano ya raia wake ili kulinda usalama wa taifa
 
Mahakama ya Rufaa ya D.C. imetangaza uamuzi wa kuunga mkono sheria inayotaka ByteDance, kampuni mama ya TikTok kutoka China, kuuza hisa zake za programu hiyo ifikapo Januari 19, 2025, la sivyo itakabiliwa na marufuku kote Marekani.
View attachment 3171068
Sheria hiyo, inayojulikana kama Protecting Americans from Foreign Adversary Controlled Applications Act, imeelezwa kuwa imelenga moja kwa moja kulinda usalama wa taifa.

Hata hivyo, TikTok imepinga hatua hiyo, ikidai inakiuka haki ya Kifungu cha Kwanza cha Katiba ya Marekani (First Amendment).

Mahakama, kwa upande wake, imesisitiza kuwa ushahidi wa serikali ya Marekani kuhusu hatari za kiusalama una uzito mkubwa, ikizingatia ushawishi wa programu hiyo duniani na uwezekano wa matumizi mabaya.

Soma, Pia: Bunge la Marekani lapitisha Muswada wa Sheria ya kuifungia TikTok
==
The U.S. Court of Appeals for the D.C. Circuit has upheld a law requiring TikTok's Chinese parent company, ByteDance, to sell its stake in the app by January 19, 2025, or face a nationwide ban.

The decision supports the Protecting Americans from Foreign Adversary Controlled Applications Act, which the court deemed narrowly tailored to address national security risks.

While TikTok argues the law infringes on First Amendment rights, the ruling emphasised the app's global reach and potential for misuse, citing the U.S. government's persuasive evidence.
If you cannot win it, buy it or close it.
Kuna kamtandao kengine ka mchina ka manunuzi huko Marekani kanashika kama moto kwa kuuza vitu bei chee. Na kanauza vitu kwa hasara ili kwanza kashike hatamu.
 
Mtandao wa hovyo, lkn Marekan nayenyewe iache soko huria liamue, au waanzishe TikTok yao nasio kufungia mitandao. Hivi Tz ikifungia watsp, X, insta wakasema sio salama kwa nchi yetu itakua sawa?.
 
Wakati wenzetu wanapigania USALAMA wa nchi yao. Hapa kwetu serikali inapambana kudukua mawasiliano ya raia wake ili kulinda usalama wa taifa
Kwaiyo unataka usalama wa taifa usilindwe?
 
Mtandao wa hovyo, lkn Marekan nayenyewe iache soko huria liamue, au waanzishe TikTok yao nasio kufungia mitandao. Hivi Tz ikifungia watsp, X, insta wakasema sio salama kwa nchi yetu itakua sawa?.
Hoja ya marekani ambayo hawaiweki wazi ni kuwa China wanaweza kutumia huo mtandao kudukua mawasiliano
Ya watu.. wanaweza wakaweka bug kwenye hiyo app..

Maana hiyo app sababu inafanya kazi na camera na audio.. ni rahs kuigeuza ikawa inarecord au kupiga picha bila
mhusika kujua

Fikiria mtoto au ndugu wa seneta au mkuu wa majeshi yuko home ana tiktokika .. na mchina wakajua kuwa ni mtoto wa mkuu wa majeshi ni rahs kuigeuza hiyo app na kuanza kuichunguza hiyo familia na kunasa mazungumzo yao
 
Hao jamaa wanaogopa ushindani na soko huria
 
Nawaza TU, Mimi SI mchumi Wala sielewi chochote kuhusu haya mambo. Hivi kama marekani anapambana hivi TikTok isiingie kwake au iingie lakini ikiwa inamilikiwa labda partially na mzawa........ Sisi serikali haiezi toza hizi APP zinatumika hapa nchini Kodi????.
Maana Kuna utitiri wa apps na pengine zingetozwa Kodi ingeleta unafuu kwenye kukusanya mapato ya serikali na kutunisha hazina ( ili waendelee kuiba na KUJAZA matumbo na mifuko...JOKING)... na hatimae kuboresha maisha na huduma kwa watanzania.
Sijui lakini.
 
Kwa Taarifa yako Marekani inadukua kila inachokiweza kutoka kwa kila mtu na kila Taifa na inadukua kila kitu kadri technology yao inavyoweza.
Thibitisha kauli yako
 
If you cannot win it, buy it or close it.
Kuna kamtandao kengine ka mchina ka manunuzi huko Marekani kanashika kama moto kwa kuuza vitu bei chee. Na kanauza vitu kwa hasara ili kwanza kashike hatamu.
Hako kanatumika kukusanya taarifa tu, hakana lingine.
 
Ila kwa mwendo wa china, vikwazo sasa vitashindwa kufanya kazi. Halafu ukweli ni kwamba hakuna kipya anachofanya china, anapita mule mule wengine walichofanya.
Mfano now anatoa offer hadi za mshahara mara 300 kwa talents kuhamia kwake, ambapo marekani na ulaya wamejipanga kumdhibiti but marekani amefanya innovations kwa miaka mingi kwa kutoa maslahi makubwa kwa talents pia.
 
Tatizo mbavu na mapafu. China kuna kipindi alihamia kwenye soka, akawa analipa pesa ndefu kufuru Sasa hivi ameshaachana nayo
 
Back
Top Bottom