Kuna aina ya mchezo imeibuka nchini hasa baada ya wachambuzi ku conclude kuwa ili kuifunga Simba unahitaji kucheza mchezo wa kutumia nguvu kupita kiasi.
Mtindo huu umeonekana kuwapa matokeo baadhi ya timu hasa kutokana na waamuzi wetu kutofuata kanuni za mpira wa miguu na kuyaachia matukio ya kurukia kwa nia ya kuvunja miguu ya wachezaji yakizidi kutokea.
Kama mpira utakuwa wa mtindo huu unaoshabikiwa na wengi wa wachambuzi wa soka,wa kuvunja ikibidi ili usifiwe kama beki mwenye "roho mbaya",basi inaweza kufanya baadhi ya wachezaji waogope kucheza kwa viwango vyao na kutafuta ligi zenye ushindani wa kweli.
Timu zinapaswa kupania kupata ushindi dhidi ya timu kubwa ila si kukomoa kwa kujaribu kuwarukia wachezaji wenzao kwa namna za hatari kwa lengo la kuwavunja ikibidi. Hii haina tija kwa mchezaji anayefanya hivyo zaidi ya kujijengea uhasama tuna mashabiki na wachezaji wenzake