Timu kubwa zaidi duniani

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
ZIJUE KLABU KUBWA NA MAARUFU ZA SOKA ZAIDI DUNIANI​

(10) JUVENTUS

Juventus: Juventus ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia kwa sasa imewekwa katika nafasi ya 10 katika orodha ya klabu maarufu zaidi duniani kwakuwa na mashabiki milioni 21 duniani kote.Hii inatokana kufanya vizuri katika michuano mbalimbali iikiwamo kuchukua kombe la ligi kuu nchini itali ikiwa ni pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya klabu bingwa ulaya ( U.E.F.A) msimu wa 2012/2013.

(9) INTER MILAN

Inter Milan ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia inatua katika nafasi ya 9 inatarajiwa kuwa na mashabiki milioni 24 duniani kote kwa sasa hii ni kutokana na kuwa moja ya klabu kongwe barani ulaya zilizojizolea mashabiki wengi duniani kote hususani kipindi ambacho ilikuwa chini ya kocha anayeaminika kuwa kocha wa kipekee (Special One) Jose Mourinho.

(8) BAYERN MUNICH

Bayern Munich ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ujeruman inakadiriwa kuwa na mashabiki milioni 50 duniani kote ambao inawafanya kushika nafasi ya 8 katika orodha ya klabu maarufu zaidi za mpira wa miguu. Hii imetokana na kufanya kwake vizuri katika ligi ya BUNDESLIGA pamoja na michuano ya U.E.F.A kwa msimu wa mwaka 2012/2013

(7) LIVERPOOL

Liverpool: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza imekuwa ukifanya vizuri kwa siku za hivi karibuni katika mashindano mbalimbali imekuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 70 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 7 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani.

(6) AC MILAN

Ac Milan: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini italia kwa sasa imewekwa katika nafasi ya 6 katika orodha ya klabu maarufu zaidi duniani kwakuwa na mashabiki milioni 98 duniani kote.Hii inatokana kufanya vizuri katika michuano mbalimbali iikiwamo kushika nafasi nne(4) za juu kwenye ligi ya italia hivyo kupata nafasi ya kushiriki ligi ya klabu bingwa ulaya ( U.E.F.A) msimu wa 2013/2014.

(5) ARSENAL

Arsenal: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na kutokufanya kwake vizuri katika michuano mbali mbali bado imeendelea kuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 115 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 5 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani na inasadikika mashabiki wengi wa klabu hii wanapatikana katika mabara ya Asia na Afrika.

(4) CHELSEA

Chelsea: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza amayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya vizuri katika michuano mbali mbali na imeendelea kujikusanyia mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 140 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 4 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani.

(3) REAL MADRID

Real Madrid: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispnia imekuwa ni klabu inayofanya vizuri kwa muda mrefu sasa na kinachovutia watu wengi duniani ni mpango wa klabu hiyo kusajili wachezaji wote maarufu duniani kama Ronaldo De Lima, David Beckham, Luis Figo, Zinedine Zidane jambo ambalo limewaongezea mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 180 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 3 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani.

(2) BARCELONA

Barcelona: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispnia imekuwa ni klabu inayofanya vizuri kwa muda mrefu sasa na kinachovutia watu wengi duniani ni mpango wa klabu hiyo kukuza wachezaji na kucheza soka maridhawa huku kivutio kikubwa kikiwa ni nyota wake wa kiargentina Lionel Messi jambo ambalo limewaongezea mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 260 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 2 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani.

(1) MANCHESTER UNITED

Manchester United: ni kabu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na kutokufanya kwake vizuri katika msimu huu wa ligi ya EPL bado imeendelea kuwa klabu mashuhuri yenye mashabiki wengi wanaokadiriwa kufikia milioni 350 duniani kote hadi hivi sasa hvyo inashika nafasi ya 1 kwa kuwa klabu maarufu zaidi duniani na inasadikika mashabiki wengi wa klabu hii wanapatikana katika mabara ya Asia na Afrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa Cha habari kingekuwa club zenye mashabiki wengi duniani na sio club kubwa Kuna tofauti ya ukubwa na umaarufu ukubwa unaendana na idadi ya vikombe walivyochukua
Unataka kuniambia liester city nikubwa kuliko Totenham. Mi nafikiri ukubwa wa timu unatokana na kuwa bora kwa misimu kazaa mfululizo. Mfano Man City zamani haikuwa timu kubwa ila kutokana na ubora wake wa misimu hii ya karibuni sasa ni timu kubwa.

Tatizo tunachanganya ukubwa na umaarufu.ukubwa una kuja na kuondoka unatokana ubora wako wa misimu kadhaa,ila umaarufu upo tu hata ukishuka daraja wewe bado upo palepale umaarufu wako hauondoki.na umaarufu unakuja kwa mfano ulibeba mataji mengi kukiko wezako,umaarufu unakuja kutokana historia.
 
Kwahiyo timu yenye mashabiki wengi ndio kubwa? Hata kama ina mafanikio finyu?
 
Sio duniani ni Ulaya. Vigezo hivyo ulivyoangalia Al Ahaly, Zamaleck, Orlando na Boca Jr wanampita inter na AC kwa mashabiki.
 
Mkuu weka source. Juventus ipo juu ya Bayern, Liverpool ipo juu ya Arsenal na Chelsea haijawahi kuizidi AC Milan
 
Sio duniani ni ulaya
Vigezo hivyo ulivyoangalia Al Ahaly ,Zamaleck ,Orlando na Boca Jr wanampita inter na Ac kwa mashabiki

Mwenyewe nimeshangaa kuna hizi timu zina mashabiki wengi sana duniani na maarufu mno,

1 Boca juniors
2 River plate
3 Al ahly
4 Zamalek
 
Mbulula yeyote anaebisha aje na takwimu zenu sio kudandia gari kwa nyuma,tatizo mnashabikia vitimu vya mfukoni mwa watu ndy maana mnatoa mipovu,eti zamalek na Al ahly are you stupid?? Africa itoe timu pendwa kuzidi timu za Ulaya?? Acheni kufikiri kwa kutumia masabuli[emoji34][emoji34]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arsenal na man u zina mashabiki wengi duniani kuliko barca na madrid. Chelsea haiwezi kuizidi ac milan kwa mafanikio wala kwa mashabiki duniani. N.b kabla ya mwaka 2003 chelsea ilikuwa levo za akina Everton na spurs...
 
Mahabbaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…