Timu mbili za Wizara ya Ardhi zafuzu hatua ya 16 bora kwenye mashindano ya SHIMWI

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Michezo inatoa fursa muhimu ya kuimarisha afya na mshikamano miongoni mwa watumishi wa umma na inasaidia kuleta hamasa kwa watumishi kufanya kazi kwa tija na uzalendo kwa taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko Septemba 25, 2024 wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo yanaendelea katika viwanja vya Jamhuri, mkoani Morogoro.

Akizungumza na wanamichezo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Seushi Mburi mara baada ya uzinduzi wa michuano SHIMIWI inayoendelea mkoani Morogoro amesema viongozi wa Wizara wanawapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye michuano hiyo na kufanikiwa kufika hatua ya 16 Bora.

Timu za mchezo wa Netboli na mpira wa miguu ndizo zimeingia hatua ya 16 bora katika mashindano hayo huku akiwapongeza wachezaji wa mchezo wa kamba kwa kuonesha upinzani mkali, na kuwataka kufanya maandalizi ili kufanya vizuri kwa msimu ujao.

Kaulimbiu ya mashindano ya SHIMIWI mwaka huu ni ‘’Michezo huongeza utendaji kazi, Shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu".
 
Nchi ina migogoro.nyie mnaenda kurukaruka na kugawana posho.

Ongezeni bidii na kuiweka ardhi salama.
 
Back
Top Bottom