Timu tatu kutoka kanda tano kuwakilisha kwenye CAF Super League

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Wadau hii nimeipata mahala nimeona ina make sense.

Kuhusu uwepo wa mashindano ya CAF Super league yatakayoanza mwakani 2023. CAF watachagua timu tatu kutoka kanda zake tano kuwakilisha kwenye hayo mashindano, kanda hizo ni Kaskazini, Mashariki, Magharibi, Kati, na Kusini.

Vigezo vya timu husika ili kuchaguliwa vitakuwa ni uwepo wa timu za vijana na wanawake zinazoeleweka, uwezo wa kiuchumi [uwekezaji], wingi wa mashabiki na uongozi unaoeleweka wenye mipango endelevu kwa timu husika.

Hapa najiuliza, itakuwa vipi kama kutokea kanda moja pakawepo na timu nyingi zinazokidhi hivyo vigezo tajwa hapo juu? Jibu langu ndio linanielekeza kwamba watatumia rankings za CAF kupata washiriki.

Anyway, lets wait and see.
 
haya mashindano kama yanaanza mwakani, basi hapana shaka tathmini ya kutafuta washiriki inaanza sasa, hasa kwa kuangalia msimu huu mpya wa mshindano mbalimbali ya mpira wa miguu (ligi kuu, caf champions, na kombe la shirikisho) na si historia
 
hapana ni .......

Kama hapo Sudan na Ethiopia Watachukuliwa ni East Africa basi tarajia, Mamelodi, kaizer chiefs, orlando pirates......simba..al hilal, el merreikh..zeco, zanaco,nkana....teama nane kusini mashariki mwa afrika ila nchi hairuhusiwi kutoa zaidi ya teams 3
 
haya mashindano kama yanaanza mwakani, basi hapana shaka tathmini ya kutafuta washiriki inaanza sasa, hasa kwa kuangalia msimu huu mpya wa mshindano mbalimbali ya mpira wa miguu (ligi kuu, caf champions, na kombe la shirikisho) na si historia
Nadhani wataangalia ubora wa vilabu kulingana na rankings zao CAF, sioni kama timu kuwa bingwa kwenye nchi yake kwa msimu mmoja inaweza kuingia huko moja kwa moja.
 
Sudan wakichukuliwa kama EA naona watatunyonya nchi nyingine nafasi zetu, Al Hilal na El Merreikh watawekwa pamoja na Simba, naona hii itaziacha timu nyingine bora kwenye ukanda huu kama Vipers wasiende.
 
Vipers sio timu bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…