Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
GEITA GOLD MABINGWA WA LIGI SOKA DARAJA LA KWANZA...
Klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi soka daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kuichapa Mbeya Kwanza bao 1-0.
Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam haukuwa mwepesi kwa timu zote kwani hadi dakika 90 zinahitimika timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa sare ya kutofungana.
Geita iliyoshiriki ligi daraja la kwanza toka kundi B ilipata goli hilo na la pekee katika kipindi cha kwanza cha dakika 30 za nyongeza.
Mbeya Kwanza ilikuwa imepigiwa chapuo ya kuutwaa ubingwa wa ligi soka daraja la kwanza lakini walishindwa kufua dafu mbele ya Geita Gold iliyojipanga vyema kwa ajili ya mchezo huo.
Timu zote mbili zimepata tiketi ya Moja kwa Moja ya kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.