PreGE2025 Timu ya Kampeni ya 'Mama Asemewe' watinga mtaani kumsemea Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kikubwa ni kuwakariri tu, hakuna marefu yasio na ncha. Zama hizi zitapita wakija wenye akili tutafanya kuwaumbua tu.
 
Hawa Chawa hawawezi kujibu HOJA za CHADEMA na ACT WAZALENDO za kwamba mfumo wa Uchaguzi hauko FAIR wala HURU unawapendelea CCM haufuati matakwa ya Watanzania.
Mambo ya Uchaguzi sio kipaombele Cha Umma Bali maendeleo
 
Kikubwa ni kuwakariri tu, hakuna marefu yasio na ncha. Zama hizi zitapita wakija wenye akili tutafanya kuwaumbua tu.
Mtawaumbua Kwa kuwa wanamsemea mama au? 🤣🤣

Kwa akili hizi ndio mnadai mnapigania ulombozi 😁😁
 
Wamefika wapi hawa? Tuwaambie ukandamizaji tunaofanyiwa wananchi huku mtaani toka kwa watendaji wa hovyo wakampelekee.
 
Isijirushe ufahamu hii Tume haitendi HAKI inawafavour CCM.

Bila HAKI hayo hakuna maendeleo ni kazi bure Nchi itangia Vitani hayo Madaraja yatabomolewa na kwenye Vita.
CCM ndio wameshika mpini
 
Kikundi hicho kimesajiliwa? Mbona polisi hawawakamati kama wale jamaa wa NETO?
 
Vijana wa namna hii katika nchi ni hatari sana.

Hivi kampeni zimeanza?

Hakuna anayetaka kufanya vurugu au kuzuia uchaguzi, kinachotakiwa ni "fair and free election"

Wazee huko CCM waambieni hawa vijana Taifa linahitaji vijana shupavu wenye kusimamia Taifa lao sio kupigania watu, Taifa linahitaji vijana wakupigania maslahi ya Taifa na watu wake na sio maslahi ya chama na wagombea nyadhifa.

CCM muache kuifanya siasa ndio ajira Kwa vijana, tunahitaji hii nguvu kazi kwenye kujenga nchi na sio kupiga blah blah mitaani.
Vijana wahivi wanapaswa kukuza upeo wao maana ukiwasikiliza tu unaoa na kugundua vichwa vyao NI empty.
 
Vijana waCDM Kesho wakianza kupitia nao mtaani na kuwaambia watu wasimchague mama maana Kwa sababu A,B,C,D nao mtawaacha.

Hawa vijana hawaoni kama kitendo cha kuachwa kupiga kampeni ndio tunasema hakuna fair and free election maana CCM inafanya kampeni na Tume ya uchaguzi imebaki inaangalia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…