Timu ya Mbwana Samata, leo kupambana dhidi ya Liverpool

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Ni mtanzania wa kwanza kucheza na mabingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya. Liverpool fc.

Ni mtanzania wa kwanza kujaribu kumfunga kipa bora wa mwaka. Alison Becker.

Ni mtanzania wa kwanza kukabwa na beki bora wa msimu, kwa klabu ya liverpool. Vrigil van Djik

Ni mafanikio makubwa kwake. Kaza buti mzee baba, utazidi kuvunja rekodi zako mwenyewe.


=======


Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu yake ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 4:00 usiku wa leo

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool unatarajiwa kuwa na msisimko wa pekee kutokana na kiu ya Watanzania kuona namna Samatta atakavyochuana na beki bora duniani kwa sasa, Virgil van Dijk.

Samatta anategemewa katika idara ya ushambuliaji ya KRC Genk, atakuwa na kibarua kizito mbele ya beki huyo ambaye amekuwa nguzo ya Liverpool kwenye safu yao ya ulinzi, akishirikiana na Joël Matip.

Je, Van Dijk ataweza kuzuia moto wa Samatta?
 
Mbwana will never walk alone. 💙💙💙
 
tumuombee afunge kwa kumpiga kipa tobo.
lakini pia tujifunza, WATANZANIA NI WANAFIKI SANA, ETI MTU ANAPINGA WACHEZAJI WA KIGENI LAKINI ANATAKA WATANZANIA WAENDE HUKO NJE
 
Mechi inaoneshwa supersport namba ngapi?
Nambieni nijue kama kifurushi changu cha Dstv naweza ona hii mechi
 
Hawa Genki wanaweza pigwa mvua. Yaani utazani wako ugenini
 
Ila Samatta namuona katulia sana anapokuwa na mpira
 
Hatujali ilimradi tu samatta atupie nyavu za liver
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…