Timu ya Polisi inastahili adhabu kali

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimeona polisi wakileta vurugu baada ya mechi na biashara. Tabia hii ni ya kulaaniwa sana kwa vile si ya kiuana michezo.

Kama TFF itawachekea, kuna sikuwa mambo yatakuwa mabaya zaidi hasa pale raia watakapoamua kuingilia ugomvi kama huo.

Sijui sheria inasemaje ila walipaswa kufungiwa kabisa kushiriki ligi inayoangaliwa na TFF. Wacheze ligi za majeshi tuone kama watafanya walichofanya mbele ya majeshi mengine.
 
Timu ya Polisi Tanzania vurugu zao wanazifanya kwakuwa Ulinzi unakuwa chini ya Polisi wenzao kitu ambacho naona kama ni Mgongano wa Kimaslahi.

TFF Fanyeni marekebisho kwenye kanuni zenu, Wakati ambaoTIMU YA POLISI Tanzania inacheza Ulinzi utolewe na SUMA JKT Au Magereza nk ili kuondoa madudu ya Kiusalama wakati wa Mechi zao lkn pia kuondoa mgongano wa kimaslahi. Timu nyingine simamieni hili suala ili kieleweke.
 
Karibu timu zote za majeshi hujifanya wababe zinapocheza na timu za kiraia! TFF liangalieni hili.
 
Si waanzishe ligi zao waache ligi za mpira na raia wa kawaida kama TFF inawaogopa.Au TFF ianzishe adhabu ya utovu wa kinidhamu kwa club yoyote inayoshiriki mchezo chini ya shirikisho lake,moja iwe adhabu ya kucheza bila mashabiki kwa timu husika iliyotenda kosa au kama ni Mchezaji basi litazamwe kosa lake ni adhabu ya kukosa mechi mbili na faini ya kiasi cha pesa.Sheria ziwe wazi vinginevyo kila miaka inavyokwenda ni makosa yale yale yanajirudia.
 
Hizi timu za jeshi na polisi zitaondolewa lini?

Hazina mashabiki, hazina msaada wowote katika uendelezaji na ukuaji wa soka la Tanzania, zinacheza mpira wa kihuni uliopitwa na wakati

Hizi timu zingetimuliwa tu zikaanzishe ligi yao wenyewe ya gwaride kama wanapenda
 
Timu za majeshi wawe na mashindano yao wakachezeshane vichura wenyewe kwa wenyewe.
Mimi binafsi nazichukia sana kwasababu ya ubabe,hawanaga fairplay.
Soka ni burudani pia ni pesa na sio mguu pande nyuma geuka.
 
Timu ya Biashara walifanyiwa vurugu kabla ya mechi na timu ya Polisi wakaenda kuripoti kituo cha Polisi.
Kesi ya Nyani anapelekewa Ngedere.
 

Kwa Kukusaidia tu hakuna Timu ambayo inaongoza kwa Kufanya Vurugu, Hujuma, Hila na Vitimbi iwapo Kwake ( Kwao ) kama Biashara United FC.

Na bahati nzuri ni Timu ya Mkoa wangu ( tena wa Kiasili kabisa ) tu ila imeshalalamikiwa na karibia kila Timu inayoenda Kucheza pale Kwao Karume Stadium.

Ukiona hadi Makocha Marafiki zangu ambao ni Wapole na Wastaarabu mno Kitabia akina Zuberi Katwila na Salvatory Edward wamewalalamikia Biashara United FC pamoja na Mashabiki wake wawapo Kwao Karume Stadium Mkoani Mara ( Musoma ) jua ni kweli na kuna tatizo Kubwa.

Kulalamika Kwao leo ni Kuzuga tu na kutaka Kutengeneza Mzani ( balance ) kuwa hata Wao pia wanaonewa kwakuwa wameshahidi kuna Kikao cha Kamati ya Nidhamu cha TFF kitakaa na kuna Adhabu Kali inaenda Kuwaangukia Biashara United FC ya Mkoani Mara ( Musoma )

Na kama kweli leo Polisi FC nao Wametembeza Kichapo Kwao Biashara United FC na Shabiki zao nawapongeza sana kwani huenda sasa na Wao ( Biashara United FC ) wakajitathmini na wakabadilika upesi. Mbona wanacheza Mpira mzuri sana tu hawa ' Mapoti ' zangu Biashara United FC sasa hizi Fujo zao ( hasa za nje ya Uwanja ) huwa ni za nini?
 
Dah Generalist gentamicin mzukulu wote wenyeji wa mkoa wa Mara na wote miandiko yenu inafanana aisee Mara mmebarikiwa Sana hongereni
 
Dah Generalist gentamicin mzukulu wote wenyeji wa mkoa wa Mara na wote miandiko yenu inafanana aisee Mara mmebarikiwa Sana hongereni

Kwani hakuwezi kuwa na coincidence ya hao Mabasha zako uliowataja hapo pamoja na Mimi Generalist wote tukawa tunatokea Mkoa Mmoja wa Mara / Musoma? Kuna Watu ni Wapumbavu na Waswahili mno hapa Jamvini. Badilikeni hamjachelewa!!
 
Kwani hakuwezi kuwa na coincidence ya hao Mabasha zako uliowataja hapo pamoja na Mimi Generalist wote tukawa tunatokea Mkoa Mmoja wa Mara / Musoma? Kuna Watu ni Wapumbavu na Waswahili mno hapa Jamvini. Badilikeni hamjachelewa!!
Aaah genta matusi ya nn Tena Wewe utakuwa popoma mwandamizi kabisa
 
Achana na Polisi kuna wale Rhino Ranger's ya Tabora balaa lake sio,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…