Timu ya soka ya Urusi yafungiwa miaka minne kushiriki michuano mikubwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Urusi imefungiwa miaka 4 kutojihusisha na mchezo wowote duniani, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya udanganyifu kuhusu vipimo na maabara juu ya utengenezwaji na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Taarifa ya Shirika la kupinga dawa za kuongeza nguvu michezoni 'World Anti-Doping Agency' (WADA) leo Desemba 9, 2019, imeeleza kuwa Urusi inatakiwa kusimamishwa na mashirikisho yote yanayosimamia michezo duniani ikiwemo FIFA kwa upande wa soka pamoja na Kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC).

Kufungiwa huko ni wazi kuwa Urusi itakosa michuano mbalimbali mikubwa ndani ya miaka hiyo ikiwemo Olimpiki 2020, itakayofanyika jijini Tokyo Japan, pamoja na FIFA World Cup 2022 nchini Qatar.

Uamuzi huu umekuja ikiwa ni miaka minne imepita tangu uchunguzi mkali uanze kufanyika, ambapo tayari viongozi mbalimbali wa michezo nchini humo, wameshafungiwa kwa hatia hizo hizo za kuhusika kuruhusu wanamichezo kutumia dawa za kuongeza nguvu.

WADA wameweka wazi kuwa Urusi kupitia maabara zao za Moscow, waligoma kuchunguzwa na baadaye walipokubali walitoa taarifa feki na kisha kufuta baadhi ya taarifa ambazo zingeeleza ukweli juu ya suala hilo.

Kwa upande wa klabu ya Saint Petersburg ambayo inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Man City kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, wao wataendelea pamoja na timu ya taifa itacheza EURO 2020 kutokana na michuano yote hiyo kuandaliwa na UEFA na sio FIFA.

Hata hivyo wamepewa siku 21 kuweza kukata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya michezo 'Court of Arbitration for Sport' (CAS).
 
Hawawezi tekeleza hiyo adhabu hadi mwisho itakuwa kama Chelsea tu
 
Mkuu kwa sasa warusi wanachukiwa sana Europe sababu kuu ikiwa ni mgogoro wake na Ukraine [emoji1255] na lile Sakata ya Uk, wameondolewa mpaka kwenye G8, Nato pia wanajiimarisha dhidi yao kila kukicha so Duniani kuna unafki mwingi sana mkuu + uongo, ukiskia wamepewa adhabu kutokana na kutumia dawa za kuengeza nguvu haimaanishi ivyo tu ila kuna mambo mengi ya kipolitics nyuma yake, kwani Iraq ilipovamiwa eti kwa sababu ya silaha za sumu ilikua ni kweli? So ujue hii Dunia ni yakinafki mno
Politics kivipi?wafungiwe na politics au ktk politics pia wanatumia madawa ya kuongeza nguvu za kisiasa!?LOL
 
Urusi ana nini kwenye michezo hadi afanyiwe figisu?! Mbona hajafanyiwa China ambaye yuko juu kimichezo kuliko Russia!
 
Fitna za kimataifa hizo, eti wameruhusu mwanamichezo kushiriki lakini sio kwa kutumia bendera wala wimbo wa Urusi....

Kwamba nikashiriki mashindano ila nisitambulike kwa namna yoyote ile... Wapuuzi kweli mabeberu hawa.!
 
Nakuunga mkono mkuu, fitna mbaya sana
Fitna za kimataifa hizo, eti wameruhusu mwanamichezo kushiriki lakini sio kwa kutumia bendera wala wimbo wa Urusi....

Kwamba nikashiriki mashindano ila nisitambulike kwa namna yoyote ile... Wapuuzi kweli mabeberu hawa.!
 
Wachache wenye akili ndio wataelewa
 
Fitna za kimataifa hizo, eti wameruhusu mwanamichezo kushiriki lakini sio kwa kutumia bendera wala wimbo wa Urusi....

Kwamba nikashiriki mashindano ila nisitambulike kwa namna yoyote ile... Wapuuzi kweli mabeberu hawa.!
Elewa kosa ni la timu ya taifa na kalifanya kwenye mashindano yanayodaminiiwa na FIFA ndio maana euro na UEFA NATION watashiriki,sasa unataka Club zifungiwe kwa zinacheza michuano yoyote ya FIFA? sawa na kosa la baba anafungwa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…